Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Mwanamvua Mrindoko akigagua Moja ya Ghala la kuhifadhia mbolea katika Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi- (Picha na George Mwigulu) |
Mkuu wa Mkoa wa Katavi
Mwanamvua Mrindoko ameyaagiza makampuni yanayosambaza mbolea Mkoani
Katavi Kuhakikisha Mbolea yote ambayo imeletwa Mkoani Katavi iwafikie
wakulima haraka iwezekanavyo ili wakulima waendelee na shughuli za kusamadia
Mazao yao Mashambani.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Mwanamvua Mrindoko akipata maelezo ya zoezi la usambazaji wa mbolea kwa wakulima kutoka moja ya Makampuni ya usambazaji wa mbolea Mkoa wa Katavi- (Picha na George Mwigulu) |
Maagizo hayo ameyatoa wakati alipotembelea na kukagua Maghala ya
Mbolea yaliyopo Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi amesema makampuni yoye
yanayoleta mbolea Mkoani Katavi wahakikishe mbolea hiyo inawafikia
wakulima kwa wakati na hato sita kuchukua Hatua kwa Makamuni yatakayo Saza
Mbollea hiyo kwenye Maghala ya hayo ya kuhifadhia mbolea pasipo na sababu
yoyote ya kutosambaza mbolea kwa wakulima.
Mrindokoa amesisitiza kuwa agizo hilo halina mjadala wala majadiliano agizo ni kutekelezwa kwa muda huo alioutowa wakulima wawe wamepata mbolea yao na kwenda nayo shambani kwa ajiri ya kwenda kutumia kwenye mazao yao waliolima shambani kwao .
Amesema kuwa msimu wa mvua Mkoa wa Katavi unawahi kuanza kuliko ilivyo kwenye mikoa mingine hivyo Mkoa wa Katavi wanachokihitaji ni mbolea kwani mvua zinaendelea kunyesha na mbolea kuendelea kukaa kwenye Maghala pasipo kuzisambaza kwa wakulima ni Kufanya Hujuma kwa wakulima nakwa Serikali ya Dk Samia Suluhu Hassan.
Ameyaonya Makampuni yanayoleta mbolea Mkoani Katavi
hawata yavumulia Makampuni yanayoleta visingizio kuwa wanashindwa kugawa mbolea kwa
kisingizio kuwa hawana sitika hali ambayo imekuwa ikisababisha uchelewashaji na
kuwafanyawakulima kupanga foleni kubwa kwa muda mrefu kwa mawakala .
Muonekano wa mbolea zilizo hifadhiwa katika Ghala la kuhifadhi mbolea zilizoletwa na serikali kupitia ruzuku kwa wakulima- (Picha na George Mwigulu) |
Mrindoko amesisitiza kuwa Onyo hilo sio kwa makampuni tu bali hata kwa mawakala au msambazaji wa mbolea amabao wamepata kazi hiyo ya usambazaji kuifanya kazi hiyo kwa mujibu wa makubaliano baiana yao na serikali.
Katibu Twala msaidizi sehemu uchumi na uzalishaji wa Mkoa wa Katavi Nehemia Jemes amesema Mkoa waKatavi kwa msimu huu wa kilimo umepangakutumia tani 14,811 kati ya tani hizo tani 7,406 ni za mbolea za kupandia na tani 74,405 ni mbolea za kukuzia ambapo mkoa umepanga kuzalisha tani 1,160,000 za mazao mbalimbali ya chakula msimu huu,
James ameishukuru serikali kuweza kutoaya shilingi Bilioni 150 kama ruzuku kwa wakulima nchinzima kwani imekuwa mkombozi mkubwa sana kwa wakulima wa Mkoa wa Katavi ambapo hadi sasa tani 6,539 zimeisha ingia shambani na kusamadia mazao ya wakulima.
Mkulima Hadson Kombe amesema wamekuwa wakipata changamoto ya uhaba wa mbolea ya kukuzia mazao huku mbolea nyingi iliyopo niyakupandia.