![]() |
Mweyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi Hamad Mapengo akiongoza kikao cha kawaida cha Baraza la Madiwani[Picha na Paul Mathias] |
Madiwani katika halamsahauri ya wilaya ya Tanganyika mkoa wa Katavi wameombwa kuwa mabalozi kwa wananchi kwenye kata zao kufanikisha wanafunzi walio chaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza wanakwenda kauanza masomo swhemu walizopangiwa.
![]() |
Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika wakiwa katika kikao cha kawaida cha Baraza la Madiwani [Picha na Paul Mathias] |
‘’Niwaombe tu
waheshimiwa kipindi hiki mtu saidie sana
Serikali watoto waliofaulu kwenda sekondari hatujawa na taarifa nzuri ya watoto
kwenda shule au kulipoti sasa naomba twende tusaidiane kwa sababu ni sehemu ya
majukumu yetu turudi kwenye kata zetu
tuhumize watendaji wa vijiji au sisi kanma kata tutafute takwimu na taarifa
rasimi zinazoonesha kwakila siku kwamba watoto waliofaulu katika secondary zetu
wangapi ambao wamelipoti nawangapi ambao hawajalipoti bahati nzuri tunazifahamu
shule zile’’ amesema Mapengo.
Mapengo amewaomba Madiwani
kuendelea kuibua Miradi ya kimukakati kwenye kulingana na mahitaji ya Kata zao
kwa lengo la kuisadia serikali inapokuwa katika mipango ya kuleta huduma hizo
kwenye kata zao.
![]() |
Watumishi wa idara mbalimbali wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika wakiwa katika kikao cha kawaida cha Baraza la Madiwani |
Kwa upande wake mkuu wa
wilaya ya Tanganyika Onesmo Buswelu amesema halmashauri lazima kuendelea kubuni
vyanzo vingi vya mapato na kusimamia vyanzo vilivyopo ili kuifanya halmashauri
kuendelea kutekeleza miradi yake kwa ufasaha.
![]() |
Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Onesmo Buswelu akitoa neno wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani Wilaya ya Tanganyika [Picha na Paul Mathias] |
Akichangia hoja mbalimbali katika kikao hicho diwani wa Kata ya Tongwe Frank Kibigas ameshauri halmashauri kuendelea kupeleka Mashne za kukusanyia Mapato POS kwenye maeneo yanayo onekana kuwa na aina ya ukwepaji wa ushuru ili kuhakikisha maeneo hayo yanachangia halmashauri kwa kazi zinazofanyika.
kwa habari zaidi tembelea ukurasa wetu wa
kataviclub.blogspot.com