RUKWA KUDHIBITI VIFO VYA WANAWAKE NA WATOTO?

 

 Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Sebastian Waryuba akiwa katika uzinduzi wa Huduma ya M-mama ambapo alimwakiisha Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Queen Sendiga kwenye uzinduzi huo
Na Israel Mwaisaka -Rukwa

Katika kuhakikisha vifo vya mama vitokanavyo na matatizo ya uzazi na vifo vya watoto wachanga vinadhibitiwa mkoa wa Rukwa umezindua mfumo wa m-mama utakaowezesha akina mama na watoto wachanga wenye dharula  wanapata huduma stakihi kwa wakati.

Wadau mbalimbali wakiwa katika uzinduzi wa huduma ya M-mama Katika mkoa wa Rukwa.
Katika kuhakikisha vifo vya mama vitokanavyo na matatizo ya uzazi na vifo vya watoto wachanga vinadhibitiwa mkoa wa Rukwa umezindua mfumo wa m-mama utakaowezesha akina mama na watoto wachanga wenye dharula  wanapata huduma stakihi kwa wakati.

Mfumo wa m-mama utahakikisha kuwa vituo vya kutolea huduma za afya vya ngazi ya chini (Zahanati na Vituo vya Afya) na wale wenye dharura waliopo kwenye jamii wanapata usafiri wa dharura utakaopatikana wakati wote.

Uzinduzi huo umefanyika  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Queen Sendiga aliyewakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Sebastian Waryuba mjini Sumbawanga ambapo amesema utasaidia kutoa huduma za usafiri wa dharura pale magari ya kubeba wagonjwa yanapokosekana .

 “Kwa sasa mkoa una magari 13 ya kubebea wagonjwa yanayofanya kazi za huduma za dharura kwa wagonjwa kwenye vituo kati ya mahitaji ya  magari 28, hivyo bado kuna upungufu mkubwa kwenye usafiri wa dharura. M-mama  ni moja ya vipaumbele katika kuokoa maisha ya wajawazito na watoto wachanga wanapokuwa na dharura za kiafya kupitia mfumo huu ” alisema Waryuba.

Waryuba aliongeza kusema mkoa wa Rukwa pamoja na kamati zake kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo umepiga hatua katika kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi kutoka vifo 74 kwa mwaka 2021 hadi vifo 47 mwaka 2022.

Washiriki katika uzinduzi wa Huduma ya M-mama katika Mkoa wa Rukwa.

 Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alizindua rasmi mpango wa usafirishaji wa dharura wa akina mama wajawazito, waliojifungua na watoto wachanga (m-mama) kitaifa  ambapo uzinduzi ulifanyika mkoani Dodoma tarehe 06 Aprili 2022 na tayari umeanza kazi katika mikoa mitano. 

Kwa upande wake Afisa Mradi wa Mpango wa m-mama Eliazal Ngage alisema mfumo huo utasaidia kupunguza vifo vya wajawazito, waliojifungua na watoto wachanga nchini kwa kuimarisha mfumo wa rufaa wa dharura kwa kutumia teknolojia ya mawasiliano ya simu kupitia kituo maalum (dispatch center).

Kwa mujibu wa taarifa ya mkoa wa Rukwa iliyowasilishwa na Mratibu wa Huduma za Afya ya Uzazi na Mtoto Asha Ressa Izina ilisema katika kipindi cha miaka mitano (2018-2022) jumla vifo 294 vya akinamama vilitokea na jumla ya vizazi hai ilikuwa 277,987.

Mratibu huyo alitaja kuwa miongoni mwa sababu zinazochangia vifo vingi vitokanavyo na uzazi  Rukwa kuwa ni kutokwa na damu nyingi kabla, wakati na baada ya kujifungua, upungufu mkubwa wa damu wakati wa ujauzito na uambukizo baada ya kujifungua, ambapo mkakati wa kukabiliana na matatizo hayo ni kuwajengea uwezo watoa huduma katika kutoa huduma za dharula kwa akina mama hao.

Mfumo huu wa m-mama unatekelezwa na Serikali pamoja na wadau wa maendeleo Vodacom/Vodafone na washirika wake Touch Foundation na Pathfinder International kuhakikisha usafiri wa dharura unapatikana kwenye vituo vya kutolea huduma za afya.

Kwa habari zaidi Tembelea Ukurasa wetu wa 

kataviclub.blogspot.com

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages