Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Mpanda kimeziomba Jumuiya za chama hicho Wilaya ya Mpanda Kubuni Miradi ya Kiuchumi itakayosaidia kujipatia Kipato na kuepuka kuwa Tegemezi katika utekelezaji wa Majukumu yake ya kila siku.
Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Mpanda kimeziomba Jumuiya za chama hicho Wilaya ya Mpanda Kubuni Miradi ya Kiuchumi itakayosaidia kujipatia Kipato na kuepuka kuwa Tegemezi katika utekelezaji wa Majukumu yake ya kila siku.Rai hiyo imetolewa na mwenyekiti wa Chama hicho Wilaya ya Mpanda Method Mtepa wakati akihutubia kikao cha kawaida cha Baraza la Umoja wa wanawake wa chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Mpanda kilichofanyika Ukumbi wa mikutano kwenye ofisi za chama hicho wilaya ya Mpanda.
Amesema viongozi hao kupitia kamati zao za
siasa za Kata wanayo Nguvu ya kuomba miradi mbalimbali ikiwemo Mashamba kupitia
kwa viongozi wao wa Vijiji ili kuanzisha miradi ya jumuiya hiyo.
‘’kuna watu mnamashamba huko mlikotoka
tunawenyeviti wetu wa vijiji na vitongoji wao ndio wamiliki wakubwa na
wasimamizi wa Aridhi hebu waambieni katika vikaovyenu ibua mawazo pale
mwenyekiti UWT tunaomba serikali ya Kijiji Itupatie eneo la kulima Karanga na
kama kamati ya siasa ikikubali maana yake mambo yanaenda vizuri”
Mtepa amesema kuwa jumuiya hiyo inayouwezo wa
kuwaelimisha wanachama na wanajumuiya kuhusu umuhimu wa kuibua miradi ndani ya
jumuiya kuanzia ngazi ya kata hali itakayo pelekea kuendelea kujenga uwezo wa
kujitemea kupitia miradi hiyo.
Amefafanua kuwa msingi wa maendeleo ya jumuiya
ni vikao na mshikamano ili kuyafikia malengo ya kuwatumikia wanachama wa chama
cha Mapinduzi CCM katika jumuiya hiyo na kukifanya chama kiendelee kuamimniwa
na wanachi kwakuwa ndicho kinacho tekeleza ilani ya chama hicho kwa sasa kwa
ridhaa ya wananchi.
Katika hatua nyingine amewaomba wanachama wa
chama hicho kuwa na utamaduni wa kulipia kadi zao za cahama ili kuonesha kuwa
wao ni wanachama hai na wasisubirie kukipia ada za uanachama kuelekea nyakati
za uchaguzi.
‘’tunalipia kadi zetu wakati wa uchaguzi uongo kweli? waheshimiwa madiwani uongo? Fomu zinatoka ndoa anaanza kujipapasa kulipia ada kwa kuwa kunakipengele kinamtaka afanye hivyo lakini kama hagombei ndo basi tena kwa hiyo kama wewe ni kiongozi hakikisha unailipia kadi yako zaidi yam waka wako wa uchaguzi’"
Katibu wa Umoja wa wanawake wa chama cha Mapinduzi CCM wilaya ya Mpanda Aziza Seirf amesema kuwa jumuiya hiyo injumla ya wanachama wapatao 9753 na matawi 144 na ongezeko la wanachama ikiwani 471.
Amesema hadi sasa jumla ya wanachama 2285 wa
jumuiya hiyo wamesajiliwa katika mfumo wa Tehama ikiwa ni sehemu ya kwenda
sambamba na maendeleo ya teknolojia na utandawazi kiutendaji unavyo elekeza
ndani ya chama.
Kuhusu kuingiza wanachama wapya Aziza
amebainisha kuwa Jumuiya hiyo kwa kipindi cha January hadi December Mwaka jana
wameweza kuingiza wanachama wapya 471
Katika hatua nyingine Katibu huyo amesema kuwa
jumuiya inao mkakati wa kuzitembelea kata na kujionea uhai wa Jumuiya hiyo
pamoja na kufanya mafunzo kwa viongozi wa kata ili kuwajengea uwezo zaidi wa
kiutendaji.Wajumbe wa umoja wa Jumuiya ya wanawake ya chama cha Mapinduzi CCM wilaya ya Mpanda wakiwa katika kikao cha kawaida cha Balaza hilo [PICHA NA Paul mathias]
Maria Magesa miongoni mwa wajumbe waliohudhuria
Baraza hilo amesema uibuaji wa miradi katika jumuiya itakwenda kusaidia usitawi
wa jumuiya hiyo na kuinua uchumi wa wanawake’’miradi ni sawa inaweza kutusaidia
kuinua uchumi wetu sisi wanawake lakini miradi tunaipata vipi tukipewa kama
mashine za kusaga zitatusaidia kuinua uchumi wetu”
Magesa amaesema umoja na mshikamano ndio
sialaha ya ushindi kwa cahama hicho kwakuwa jumuiya hiyo ndio Dira kwa chama
hicho kwa kuwa na kundi kubwa la wapigakura hasa wanawake.
Mwanahamisi Amani mjumbe wa kikao hicho
amebainisha kuwa hawatamwangusha mwenyekiti wao katika kuibua Miradi ndani ya
jumuiya hiyo kwa kuwa kunaabaadhi ya kata zimeanza kuandaa miradi yao na
vikundi mbalmbali vya kiuchumi vilivyoanzishwa na akina mama.
Amesema niwakati muafaka sasa kwa wanawake wa jumuiya hiyo kujituma na kufanya kazi kwa bidii kwa kukiendeleza chama na kuyafikia malengo yaliyokusudiwa.
Kwa habari zaidi endelea kutembelea ukurasa wetu wa
kataviclub.blogspot.com