UK aid YA MWAGA MABILIONI ELIMU MSINGI


Raymond Kanyambo Mratibu wa Mradi wa Shule Bora akitoa Mafunzo kwa waandishi wa habari Mkoa wa Katavi Kuhusu utekelezaji wa Mradi wa Shule Bora Katika Mkoa wa katavi[Picha na Paul Mathias]
Na Paul Mathia-Katavi.

Serikali ya Uingereza kupitia Shirika la UKaid kwa kushirikiana na serikali ya Tanzania limeanza kutekeleza Mradi wa Shule Bora katika mikoa Tisa Hapa nchini.

Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa Habari Mkoa wa Katavi Walter
Mguluchuma katikati akiwa katika mafunzo ya Mradi wa Shule Bora wa kwanza kushoto Anna Sawasawa afisa elimu kwa wanafunzi wenye Mahitaji Maalumu Manispaa ya Mpanda  akiwa katika mafunzo ya utekelezaji wa Mradi wa Shule Bora 
[Picha na Paul Mathias]

Serikali ya Uingereza kupitia Shirika la UKaid kwa kushirikiana na serikali ya Tanzania limeanza kutekeleza Mradi wa Shule Bora katika mikoa Tisa Hapa nchini.

Akizungunza wakati wa Semina elekezi ya Kuutambulisha Mradi huo kwa waandishi wa Habari wa Mkoa wa Katavi Katika ukumbi wa Mikutano wa Idara ya Maji Mpanda Mjini .

George Mtawa Msimamizi wa Mradi wa Shule Bora kwa Mkoa wa Katavi Amesema Mradi wa Shule Bora una malengo makuu manne ambayoni Kujifunza, Kufundisha, Jumuishi na Kujenga Mfumo.

Msimamizi wa  Mradi wa Shule Bora Mkoa wa Katavi George Mtawa akitoa mafunzo kwa waandishi wa Habari Mkoa wa Katavi namna Mradi wa Shule Bora unakwenda kutekelezwa Katika Mkoa wa Katavi[Picha na Paul Mathias]

Mtawa amesema Kwa ujumla malengo hayo yatakuwa na hakikisho la watoto wa Darasa la awali hadi Darasa la Saba wanasoma hadi Darasa la Saba wanasoma  pasipo na mdondoko wa wanafunzi kwenye masomo yao.

Amefafanua kuwa katika mradi wa Shule Bora watahakikisha watoto wote wanakuwa katika mazingira salama na rafiki ili kuwawezesha kuendelea na elimu ya msingi hadi sekondari,

Mradi huo wa Shule Bora umeanza kutekelezwa mwaka 2021-hadi 2027 kwa ufadhili  wa serikali ya Uingereza kupitia mfuko wa UK aid utakao Gharimu kiasi cha paundi za Uingereza Milioni 89 sawa na shilingi za kitanzania Bilioni 271.

wadau mbalimbali wakiwa katika mafunzo ya utekelezaji wa Mradi wa Shule Bora katika mkoa wa katavi[Picha na Paul Mathias].

Awali akitoa utambulisho wa Mradi huo kwa waandishi wa Habari mkoa wa Katavi Raymond Kanyambo Mratibu wa Mradi wa Shule Bora

Amesema wameamua kushirikiana na Kundi la waandishi wa Habari  katika mradi huo kwa lengo la kuyafikia malengo ya utoaji wa elimu katika mazingira safi kwa wanafunzi wa Awali hadi Darasa la Saba katika ngazi ya shule za Msingi hapa nchini ikiwemo mkoa wa katavi.

“tumeamua kwa watu wachache ikiwemo waandishi wa habari kuwa miongoni mwao kwa kuutambulisha Mradi wa Shule Bora  kwao  kwa kutambua kuwa vyombo vya habari vinawafikia watu wengi kwa muda mfupi’’alisema Mratibu Kanyambo

Raymond amebainisha kuwa kufanya kazi na waandishi wa Habari kuna umuhimu mkubwa kwakuwa wana uwezo katika kupambanua mambo na kuongea na jamii kupitia Habari, vipindi pamoja na makala wanazoziaandaa kwa jamiikupitia vyombo vyao vya Habari hali itakayosaidia kufikisha ujumbe huo wa Mradi wa Shule Bora kwa ulahisi kwa wananchi.

Waandishi wa habari wa mkoa wa katavi wakiwa katika mafunzo kuhusu Mradi wa shule Bora [Picha na Paul Mathias]

Zilpa Joseph Mwandishi wa Habari kutoka katavi akichangia katika kuelekea utekelezaji wa Mradi huo wa Shule Bora ameomba kuwepo na ushirikiano wa utaoji wa taarifa kwa mamlaka ili kwenda kufanikisha mradi huo kwa ufasaha.

Kwa upande wake Alex Ngereza Mwandishi wa Habari wa Radio free afrika na Star Tv ameshauri kuwa na  mazingira mazuri ya kikazi baina ya watendaji wa serikali kutokuwa na Mlolongo wa kupata habari kwenye Mradi wa Shule Bora.

“ unamkuta mtendaji wa Serikali anakubali tatizo lipo ila anakwambia hili sina mamlaka nalo mpaka nipate kibali toka juu hali hii huvunja nguvu waandishi katika majukumu yao’’alisisitiza Ngereza

Mradi wa Shule Bora unatekelezwa katika Mikoa Tisa Hapa nchini ambayo ni Katavi,Kigoma,Rukwa,Simiyu,Dodoma,Mara,Pwani, na Singida.

Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Katavi wakiwa katika mafunzo elekezi juu ya utekelezaji wa Mradi wa Shule Bora[ Picha na Paul Mthias]

Katika Mradi wa Shule Bora Jumla ya Shule za Msingi  zipatazo 5,757  nchinzima zitakwenda kunufaika na Mradi huo huku halmashari 67 zitakwenda kuwa wanufaika na mradi wa Shule Bora hali kadhalika wanafunzi 54000 nchinzima watakuwa Sehemu ya Mradi wa Shule Bora.

Katika hatua nyingine waandishi wa Habari kwa ujumla wamesema mradi huo wa Shule Bora unakwenda kuwa Mkombozi kwa jamii kwa kuisadia serikali katika kuinua kiwango cha Elimu kwa watoto wa Darasa la awali hadi Darasa la Saba kwa shule za msingi  katika mkoa wa Katavi na Tanzania nzima kwa ujumla.

 Kwa habari zaidi Tembelea katika ukurasa wetu wa 

kataviclub.blogspot.com

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages