Washiriki mbalimbali wa kikao kazi cha kuboresha Elimu ya Msingi na Sekondary kilichofanyika katika ukumbi wa Mpanda Social hall Manispaa ya Mpanda mkoa wa Katavi.[ Picha na Paul mathias]
Wizara ya TAMISEMI wamekusudia kuandoa tatizo la wanafunzi wa Shule za Msingi linalo wakabili la kutojua kusoma na kuandika na wanafunzi wanao maliza kidato cha nne kutojua kuzungumza lugha ya kingereza .
Amebainisha
kuwa kumekuwa na tatizo la wanafunzi wa Shule za Msingi
kutojua kusoma nakuandika hali ambayo imepelekea kuna Shule moja ya
Msingi hapa nchini kukosa kuwa na darasa la tano kufuatia wanafunzi wote wa
darasa la nne kufeli mtihani .
Amefafanua
kuwa hata kwenye Shule za Sekondari kumewepo na changamoto ya
baadhi ya wanafunzi wanao maliza elimu ya kidato cha nne kutojua kuongea lugha
ya Kingereza .
Kayombo amesema kuwa TAMISEMI wamekusudia kuondoa tatizo la watoto kutojua kusoma na kuandika kwenye shule za Msingi na kwenye Sekondari kuzungumza Kingereza wanaamini kuwa hilo lina wezekana .
Amesisitiza
kuwa kuanzia sasa walimu wanao kuwa wanafundisha watoto wa darasa la kwanza na
lapilli wawe ni wale wenye nguvu kuliko ilivyo sasa jukumu hilo wameachiwa
walimu wazee kwa kile kinachoelezwa wakacheze na watoto .
Pia
walimu wanaofundisha darasa la saba wawe wanashuka kufundisha hadi darasa
la tatu kuliko ilivyo sasa wanafundisha madarasa ya juu tuu.
Kuhusu
elimu ya Sekondari ameeleza kuwa kuna changamoto ya wanafunzi mpaka
wanamaliza kidato cha nne unakuta wanakuwa hawajuwi kuongea lugha ya Kingereza
Kayombo
amesema kuwa swala la kusisitiza wanafunzi wajuwe lugha ya kingereza sio
kwamba wanauwa lugha ya Kiswahili bali wanatekeleza Sheria ya Elimu ya waka 2014.
Hivyo
kuanzia sasa walimu wote wa Shule za Sekondari pamoja na wanafunzi wao lazima wawasiliane kwa
lugha ya kingereza .
Amesisitiza
kuwa hata Diwani akifika shuleni kutembelea nae apewe maelezo kwa lugha
ya kingereza na Maafisa elimu Kata wanapokuwa wanakwenda kukagua ukaguzi wao
wafanya mazungumzo kwa kutumia lugha ya kingereza tuu.
Mkuu wa
Mkoa wa Katavi amewataka walimu waeshimu maadili kwani kufanya hivyo
watakuwa wameimarisha elimu .
Katibu
Tawala wa Mkoa wa Katavi Hassan Lugwa amesema kuwa hadi sasa kati ya wanafunzi
14.904 waliochaguliwa kuanza kidato cha kwanza ni wanafunzi asilimia 25 tuu
ndio wameisha ripoti shuleni .