Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko ameagiza wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza 2023 ambao hawaja ripoti shule kwa kukosa sare wapokelewe mara moja shuleni wakati wazazi wao wanajiandaa kuwatafutia mahitaji yao .
Vile
vile amewaagiza viongozi wote wa Serikali kuanzia wa ngazi za Mitaa
,Vijiji Kata na Wilaya zote za Mkoa wa Katavi
kuakikisha kuwawasaka wazazi na watoto wa wanafunzi ambao hadi Januari 20
watakao kuwa hawaja ripoti shule.
Mrindoko
ametowa maagizo hayo wakati alipokuwa akiwahutubia washiriki wa kikao kazi cha
kuboresha ubora wa elimu wa shule za msingi na Sekondari katika Mkoa wa Katavi
.
Amesema
hadi sasa kati ya wanafunzi Zaidi ya elfu kumi nan ne waliochaguliwa kujiunga
na masomo ya kidato cha kwanza kwa 2023 ni asilimia 25 ndio wamelipoti .
Hivyo
kusiwe na sababu za watoto kushindwa kulipo shule kwa kukosa sare kwa
hiyo kwa mtoto ambae hajaripoti shule kwa kukosa sare
amepokewe shuleni hata kama hana sare za shule na badala yake
watumie hata sare walizokuwa wakivaa wakiwa shule ya msingi wakati ambao wazazi
wao wanaendelea kuwatafutia mahitaji yao .
Amewagiza
viongozi wote wa Serikali katika Wilaya zote za Mkoa wa Katavi
kuhakikisha wanawasaka wazazi na wanafunzi wa watoto ambao hawajaripoti
shuleni wawasake hata kama watakuwa wamejifisha juu ya miti .
Mrindoko
amewataka kila mwalimu azingatie maadili na wawatunze wanafunzi
wao wasiwafanyie vitendo vya ukiukwaji wa maadili .
Kwani
wapo baadhi ya walimu wamekuwa na tabia ya kufanya mapenzi na wanafunzi
wao wanao wafundisha na wengine wamekuwa wakiwafanya wanafunzi wake zao .
Ameagiza
walimu wote wanaofanya hivyo waache mara moja kwani hayo sio
maadili na watakao bainika hatua kali zitachukuliwa dhidi yao .
Katibu
Tawala wa Mkoa wa Katavi Abbas Hassan Rugwa amesema kuwa amesema
kumekuwepo na changamoto ya madarasa kwenye shule za
msingi kutokana na ongezeko la watoto na utolewaji wa elimu bure .
Ambapo kwa Mkoa huu madarasa yalipo ni 5,289 huku upungufu wa madara ukiwa ni 3800 hali ambayo inafanya wakati wa masomo wanafunzi wanakalishwa chini wakati wa masomo ili nafasi ipatikane .
Mkurugenzi
wa usimamizi elimu wa Tamisemi Vicent Kayombo amesema kuwa nia ya
TAMISEMI ni kuhakikisha elimu ya shule za msingi na sekondari zinaboreshwa .
Ameeleza
kuwa na ndio maana Tamisemi wameitisha kikao kazi hicho ili kuwepo na
uwelewa wa pamoja kwenye kusimamia elimu kuanzia shule za Msingi hadi
Sekondari .