wakazi wa Kijiji cha Milala wakiwa katika mazishi ya Dreva Bodaboda Marehemu Alex Lutana alifariki kwa Ajali [Picha na George Mwigulu] |
Na Paul Mathias- Katavi
Baadhi
ya wananchi katika kijiji cha Milala Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda mkoa wa
Katavi wamewatuhumu Asikari wa Jeshi la uhamiaji kwa kusabisha kifo cha Mwendesha Bodaboda kwa Kugogwa na Bus la
Adveture wakati wakimfukuza kwa kumshakia kuwa alikuwa amebeba raia wa kigeni.
waombolezaji katika msiba wa Boda Boda alex Lutana wakiwa eneo la makaburi kijijini Hapo[ Picha na George Mwigulu] |
Baadhi ya wananchi katika kijiji cha Milala Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda mkoa wa Katavi wamewatuhumu Asikari wa Jeshi la uhamiaji kwa kusabisha kifo cha Mwendesha Bodaboda kwa Kugogwa na Bus la Adveture wakati wakimfukuza kwa kumshakia kuwa alikuwa amebeba raia wa kigeni.
Philipo
Kachila mkazi wa kijiji cha Milala amesema kuwa kijana huyo akiwa anatokea
kijijini hapo alipofika eneo la ukaguzi wa kuwabaini wahamiaji haramu alianza
kufukuzwa na asikari hao kwa kutumia gari lao bila kujua kiini cha kumfukuza na
ndipo katika harakati za kuwakwepa ndipo Bus hilo likiwa mwendokasi na kumgonga
na kufariki Dunia hapo hapo .
‘’Wakati Bus la Adveture linakaguliwa boda huyo alipita akiwa amebeba watu wawili baada ya kuwa amepita hapo wale asikakari wa uhamiaji walidhani amebeba wahamiaji haramu ndipo walianza kuwafukuza hadi eneo la Milupwa Marehemu akiwa katika kuwakimbia askari hao inadaiwa alivutwa shati hari ambayo ilimfanya Bodaboda kuhaamia upande wa pili wa barabara na ndipo alikutana na Bus la Adveture na kumgonga ’’amesema kachila
Ndipo walipokuta ajali hiyo imetokea chanzo kikiwa ni kufukuzwa Bodaboda huyo na askari wa uhamiaji.
‘’tulipata taarifa hii majira ya mchana tukio ambalo limetusikitisha wanakikiji wa Milala kuna Boda boda mkazi wa Kijiji ca ha Milala alikuwa amebeba watu wake toka Milala kuja nao Mjini lakini baada ya kufika eneo ambalo Asikari walikuwa wanalifanyia ukaguzi Bus la Adveture wakahisi Boda bod huyo amebeba wahamiaji Haramu matokeo yake wakaanza kumfukuzia walipofika milupwa ndpo asikari huyo wa uhamiaji akiwa kwenye gari lake alifungua Dirisha na kumfuta shati Boda boda huyo bodaboda huyo alitaka kugeuka upande wa pili ndipo allgongwa na Bus la Adventure na kusabisha kifo cha Alex Lutana amabe ni Mwendesha Boda Boda’’
Kwa
wake shemeji wa Malehemu Kabona Gibson
Mkazi wa Milala amebainisha kuwa alipata taarifa ya ajali hiyo majiara ya saa
nne asubuhi na kwenda eneo la ajali hiyo ndipo alipokuta ndugu yake akiwa
amefikwa na umati na mwenzake akiwa amejeruhiwa vibaya.
Katika
hatua nyingine wananchi hao wamesema kuwa tukio hilo litakuwa la mara ya pili
kwani kuna tukio la aina kama hilo la bodaboda kufukuzwa na Asikari wa uhamiaji
lilitokea ingawa halikusabisha kifo.
Wakazi wa kijiji cha Milala wakielekea eneo la Makaburi kwaajili ya mazishi ya Dreva Boda Boda Alex Lutana alifariki Dunia kwa ajali ya Barabarani [Picha na George Mwigulu] |
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi Ali Hamad Makame amekili kutokea kwa kifo hicho na kuahidi kutoa taarifa zaidi juu ya tukio hilo baada ya uchunguzi wa kina kufanyika.
‘’nikweli
imetokea hiyo ajali nyakati za mchana ililipotiwa kwamba huyo kijana wa Boda
Boda alipita hapo aliposimamishwa na watu wa uhamiaji hakutii lile agizo na
kukimbia huku akiwa na mashaka akiwa katika hali ya kugeuka ndipo alipokutana
na ajali hiyo na kuingia uvunguni na hayo nimatokeo ya Boda boda kukataa
kusimama kwenye eneo la ukaguzi” amesema kamanda Makame.
Kuhusu
uwepo wa mkimbizano baina ya Asikari hao na Bodaboda huyo kamanda makame
wanaendelea kufanya uchunguzi juu ya hilo na watatoa taarifa kwa umma.
‘’tukishasema
tunachunguza maana yake yote hayo tutakuja kuyabaini lakini kwanza turipoti
hilo kama tutabaini kunajambo jingine basi hatutasita kuendelea kutoa taarifa
juu ya hilo’’
kwa habari zaidi tembelea ukurasa wetu wa
kataviclub.blogspot.com