BODA BODA MSIVAE KOFIA ZA WAKANDALASI WA TANESCO


Willy Mwamasika Mkuu wa Usalama Barabarani Mkoa wa Katavi akizungumnza na waendesha pikipiki maalufu kama Bodaboda juu ya namna bora ya kuzingatia sheria za usalama barabarani na usalama wa vyombo wanavyoviendesha[Picha na Paul Mathias]
Na Paul Mathias -Katavi.

Waendesha Pipiki Maalufu kama Boda boda katika Mkoa wa Katavi wameonywa kutokuwa sehemu ya kufanikisha vitendo vya uhalifu na wahalifu katika shuhguli hiyo wanayoifanya kwenye Jamii.

Waendesha pikipiki maalufu kama Bodaboda Katika Mkoa wa Katavi wakiwa katika semina ya kujengewa uelewa juu ya sheria za usalama barabarani na usalama wa vyombo wanavyoviendesha[Picha na Paul Mathias]

Waendesha Pipiki Maalufu kama Boda boda katika Mkoa wa Katavi wameonywa kutokuwa sehemu ya kufanikisha vitendo vya uhalifu na wahalifu katika shuhguli hiyo wanayoifanya kwenye Jamii.

Wito huo umetolewa na mkuu wa Usalama Babarabani mkoa wa Katavi Sp Willy Mwamasika wakati akizungumnza na waendesha pikipiki katika ukumbi wa mikutano wa Polisi Mjini Mpanda , katika kukumbushana masuala mbalimbali yanayohusu usalama barabarani kwenye shughuli zao.

Mwamasika amesema kuwa kumekuwa na baadhi ya waendesha pikipiki yaani bodaboda kujiingiza katika vitendo vya uhalifu na miongoni mwao kufanikisha uhalifu kupitia kazi yao hiyo hali ambayo si njema mbele ya jamiii na taifa kwa ujumla.

Waendesha pikipiki maalufu kama Bodaboda mkoa wa katavi wakisiliza elimu kuhusu masuala ya usalama barabarani [Picha na Paul Mathias]

“niwaase wachache wanao jihusisha na Vitendo vya uhalifu na kufanikisha vitendo vya uhalifu kuacha kuwa sehemu ya matukio hayo kwakuwa nyie mnafanya kazi nzuri ya kuasafirisha abiria haipendezi kukuona upo katika kundi la kufadhili au kufanikisha uhalifu kwenye jamii’’amesema mwamasika

Amesema serikli inatambua umuhimu wa Vijana hasa waendesha Boda Boda kwa kuwa sehemu Rasimi kwa kujiaajili katika kazi hiyo ya uafisa usafirishaji kwa lengo la kujipatia kipato na kupunguza wimbi la changamoto ya ajila kwa vijana.

‘’niwaombe sana chombo hiki kama maafisa usafirishaji kimerasimishwa na serikali kama sehemu kubwa sana ya kuwapatia vijana ajira na wote hapa mmeshajiajili hakuna kitu kibaya kama mtu anakuja kuchezea ajila yako ambayo inakupa wewe liziki ya kuishi pamoja na familia yako kazi yetu hii ya bodaboda ndio inaotupa liziki’’ amebainisha

Awali akitoa neno kwa waendesha pikipiki hao mkuu wa usalama barabarani Wilaya ya Mpanda ASP Effeso Sukunelo amewaonya baadhi ya bodaboda hao kutovaa kofia ngumu zinazitumiwa na wakandalasi na mafundi kutoka shirika la umeme Tanzania Tanesco kwa kuwa kofia hizo ni maalumu kwaajili ya shuguli hizo na sio kwaajili ya kazi yao ya Bodaboda.

‘’hakikisheni mnavaa Kofia ngumu kama huna nenda Dukani kanunue na sio kunivalia Kofia za wakandalasi mmegeuka sasa hivi mnanunua kofia ngumu wengi wenu mnakofia ngumu zinazotumiwa na wakandalasi wa Tanesco mnavaa kuanzia leo kama unayo kaisalimishe kule na nunua kofika ngumu inayojulikana katika kazi yako”

Sukunelo amesema ajali nyingi zimekuwa zikisabishwa na ulevi,mwendokasi na kutozingatia alama za usalama barabarani hali ambayo imekuwa ikigharimu uhai wa watu na watumia vyombo vya moto.

Baadhi ya waendesha Pikipiki Bodaboda wakiwa katika hali ya utulivu wakati wakipatiwa semina ya masuala ya usalama Barabarani.

Jafety Andrea Mwakalabo Mwenyekiti wa chama cha waendesha pikipiki Mkoa wa Katavi amesema wao kama chama wataendelea kushirikiana na jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani kwa kuendelea kutoa elimu ya uasalama barabarani kwa Bodaboda.

Mwakalambo amewaasa vimgozi wa vijiwe vya Bodaboda kuwa na utamaduni wa kutoa taarifa za ujio wa wageni wanaofanya kazi hiyo hiyo ya boda ikiwa ni sehemu ya kuzibiti vitendo viovu vinavyolipotiwa kwa kuhusishwa na kundi la Bodaboda.

Nemesi Afled Dereva Boda katika mkoa wa Katavi amesema semina hiyo ya kuwajengea uwezo juu ya masuala ya usalama barabarani itakuwa chachu kwao kwa kufanya kazi yao kwa kuzingatia kanuni za usalama barabarani na kutambua kuwa wao ni sehemu ya jamii inayotegemewa na familia zao.

kwa habari zaidi tembelea ukurasa wetu wa 

kataviclub.blogspot.com

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages