BHSF YAHIMIZA WAZAZI NA WALEZI KUWAFICHUA WATOTO WENYE ULEMAVU

 

Mkurugenzi wa Taasisi ya Blessed Haert Foundation,Songambele Thomas Otaru akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wazazi wenye watoto wenye wenye mahitaji maalumu waliofika ofisini hapo 

Na Paul Mathias,Mpanda.

Wananchi katika mkoa wa Katavi wameaswa kutowaficha watoto wenye Changamoto maalumu katika jamii ilikuendelea kuwa na jamii yenye usawa bila kujali jinsia na mahitaji yao.

Mkurugenzi wa BHSF, Songambele Thomas Otaru akizungumnza na waandishi wa habari 

Wananchi katika mkoa wa Katavi wameaswa kutowaficha watoto wenye Changamoto maalumu katika jamii ilikuendelea kuwa na jamii yenye usawa bila kujali jinsia na mahitaji yao.

Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Blessed Heart Songambele Foundation, Songambele Thomas alipokuwa anazungumnza na waandishi wa habari kwenye ofisi za taasisi hiyo inayojishugulisha na kulea watoto wenye tatizo la ulemavu ambapo amesema jamii ya mkoa wa Katavi kwa kushirikiana na serikali kwa pamoja lazima kuungana kwa pamoja ili kuwafichua watoto wenye ulemavu kwakuwa watoto hao wanahaki ya kupata haki zote kama watoto wengine.

‘’nilikuwa naomba tushirikiane wazazi ndugu jamaa na malafiki kupitia makanisa misikiti mikusanyiko yeyote tuwaambie wanajamii watoto hawa wanasaidika wawalete tuwasaidie tunania ya kuwasaidia watoto pale walipo kwama waweze kukaa kama watoto wengine na kaulimbiu yetu Rudisha tabasamu liilopotea  Songambele”

Amesema kuwa hadi katika mkoa wa Katavi kituo hicho kimeweza kuwapokea zaidi ya watoto 40 wenye changamoto ya ulemavu na kati ya hao tayari wameweza kuwapeleka watoto Tisa kwenye Matibabu ambao walipelekwa mwaka jana mwezi wa 12 na mwaka huu wameweza kupeleka watoto wawili.

‘’tumeweza kuwafikia watoto takribani 40 na zaidi lakini miongoni mwa watoto hao tumeshafanikiwa kuwapeleaka watoto 9 kwenye Matibabu KCMC mwezi wa 12 tulipeleka watoto 7 Mwaka huu tumepeleka watoto wawili kwenye matibabu hayo.

Rehema Rashidi mzazi wa mtoto mwenye changamoto amebainisha kuwa taasisi ya Songambele FOUNDATION imeweza kumsaidia mtoto wake na alijihisi kukata tamaa kabla ya kuifahamu taasisi hiyo.

‘’kabla sijaifahamu Blessed Heart songambele Foundation nilikuwa napoteza matumaini na nilijua kwa sababu mwanangu ni Mlemavu na hawezi kuendelea lakini kwa sasa hivi namushukuru mungu nina matumaini anatoka sehemu moja na kuendelea hatua nyingine’’amenena Rehema.

Afisa Ustawi wa Jamii Manispaa ya Mpanda Khadija Said akitoa neno kwa jamii kupitia waandishi wa habari kuendelea kuelimisha jamii juu ya watoto wenye uhitaji maalumu katika jamii

Khadija Said Afisa Ustawi wa Jamii Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda amsema Taasisi ya Blesed Heart Songambele Foundation tangua ianzishwe imeweza kuwasaidia wazazi wenye changamoto hizo kwa watoto wao na kuwapeleka kwenye kituo hicho ili kuwapatia msaada zaidi wanaohitaji.

“wazazi wengi katika halmashauri ya Manispaa ya Mpanda walikuwa hawajui nisehemu gani ambayo wanaweza kuwapeleka watoto wao wenye changamoto kama hizi kwa hiyo baada ya kuja Blessed Foundation imetusaidia kwa kiasi kikubwa watoto wengi sasahivi wamepata matuamaini na ndio maana sisi kwa kushirikiana na afisa lishe tunakuja hapa kuonana na wazazi wenye watoto wenye changamoto hii”amesema Khadija.

Pamoja na hayo ametoa rai kwa jamii kuendelea kuwafichua watoto wenye mahitaji maalumu ili serikali na wadau mbalimbali amabao wameamua kujitoa kuwasaidia watoto kama hao waweze kuwasaidia kwa kuwapatia matibabu na hatimae kuendelea na maisha yao kama kawaida.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages