DKT BAGANDA NI KAZI BURE KAMA KIJANA HAJAUGANISHWA KWENYE UZALISHAJI.


Sikauti wa Mkoa wa Katavi wakifanya majaribio ya vitendo ya kuzima moto kwenye siku ya kumbukumbu ya kuanzishwa Sikauti ambayo Kimkoa yameadhimishwa katika uwanja wa shule ya msingi Kashauriri Manispaa ya Mpanda Mkoani humo.

Na Paul Mathias,Katavi.

Wazazi na walezi katika mkoa wa Katavi wameshauriwa kuwekeza katika elimu ya kujigemea kwa watoto wao ikiwa nisehemu ya kukabiliana na changamoto ya Ajila kwa vijana ambayo inaonekana kuwa tatizo kwa sasa.

Dkt Elipidius Baganda.Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Katavi akihutubia wananchi kwenye kumbukumbu ya kuanzishwa kwa chama cha Sikauti.

Wazazi na walezi katika mkoa wa Katavi wameshauriwa kuwekeza katika elimu ya kujigemea kwa watoto wao ikiwa nisehemu ya kukabiliana na changamoto ya Ajila kwa vijana ambayo inaonekana kuwa tatizo kwa sasa.

Hayo yamebainisha na Mwakilishi wa  mkuu wa Mkoa wa Katavi Dk Elipidius Baganda wakati akitoa hutoba kwa Wanachama wa Scout Mkoa wa Katavi katika maadhimisho ya kukumbu ya Mwasisi wa Scout Sir Burden Paul yaliyofanyika katika viwanja vya shule ya Msingi kashaulili Manispaa ya Mpanda.

Dk Baganda amesema kuwa wazazi na walezi wanapaswa kuwa mfano kwa vijana wao kwenye malezi yao ya kawaida kuwafundisha elimu ya kujitegemea ikiwa ni sehemu ya kuwapatia ujuzi vijana hao wa kujitegemea wanapofikia katika Umri wa kujitambua kama ambavyo vijana wa scout mkoa wa Katavi wanavyofundishwa katika mafunzo mbalimbali.

Sikauti Mkoa wa Katavi wakifanya maonesho ya  mfano wa meza iliyotengezwa na vijana hao.

‘’duniani fanya vyovyote lakini kama kijana  hajaunganishwa kwenye kuzalisha inakuwa kazi bure pale unapounganisha unachokifanya na kuzalisha hapo ndo unakuwa umecheza vizuri na pale mtakapo zalisha vijana wengi wenye ujuzi vijana hawa watakwenda kuutumia ujuzi huo kujitegemea kuwafundisha wengine hata wao kuweza kumudu uchumi na ndio maana mwalimu nyerere mwaka 1967 alianzisha Elimu ya kujitegemea” amesema Dk Baganda.

Amebainisha kuwa serikali ya Mkoa wa Katavi inatambua mchango wa chama cha Scout kwakuwa wamekuwa wakishiriki katika shuguli mbalimbali za kiserikali kwa kuzingatia weledi na uzalendo kwa kutambua kuwa wao ndio vijana wanaotaegemewa na taifa katika siku za usoni.

Kamishina wa Chama Cha Sikauti Mkoa wa Katavi,Clavery Choma akihutumbia wananchi waliohudhuria hafla hiyo.

Kamishina wa Scout Mkoa wa Katavi Clavery Choma amesema kuwa katika kumbukumbu hiyo wameweza kufanya mambo mengi kama Scout kwa kuonyesha umahili na ukakamavu kwa vijana wao zaidi ya 500 ambao wameweza kushiriki kumbukumbu hiyo na kuiomba serikali kuendelea kuwatumia vijana wa Scout kwakuwa ni sehemu ya kuonyesha uzalendo kwa taifa lao kupitia kazi mbalilmbali za serikali.

‘’sisi kama Scout katika mkoa wa Katavi tutumieni katika shughuli za kiserikali tunafanya kazi kubwa lakini malipo yetu ni kidogo kwakuwa tunatambua umuhimu wa kuwa wazalendo na tumekuwa tukiwafundisha vijana uzalendo kwa kulipenda taifa lao’’Amesema Choma.

Kamanda Jeshi la zimamoto Mkoa wa Katavi Regina Kaombwe akitoa salamu kwa vijana katika kumbukumbu hiyo amesema kuwa vijana wanapaswa kuepuka kuiga tamaduni zisizofaa ambazo zhaziendani na maadili ya kitanzania ili kuendelea kuimalisha utamaduni wa kitanzania.

Sikauti wa Mkoa wa Katavi wakiwa kwenye maandamano wakati wa  kumbukumbu ya kuanzishwa Sikauti ambapo Kimkoa yamefanyika Uwanja wa shule ya msingi Kashauriri.

“ninacho waomba mzingatie maadili na tamaduni za kitanzania mko kwenye mikusanyiko huko achaneni na mambo ya bala la Ulaya ushoga na vitu vingine msiwe navyo mko hapa kwa kuonywa na kufundishwa na kuelekezwa myazingatie yote mnayo fundishwa na kuonywa” amefafanua Kaombwe.

Katika kumbukumbu hiyo ya kuazishwa kwa Scout Duniani katika mkoa wa Katavi yamefanyika katika viwanja vya shule ya Msingi kashaulili na kuhudhuliwa na vijana wa Scout mkoa wa Katavi wapatao zaidi ya 500.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages