Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Mwanamvua Mrindoko akihutunia wajumbe wa kikao cha kamati ya ushauri ya Mkoa (RCC) katika ukumbi wa Mikutona wa manispaa ya Mpanda iliyofanyika hivi karibuni-(Na picha na George Mwigulu) |
Na Walter Mguluchuma, Katavi.
Mkoa wa Katavi katika kukabiliana na tatizo la upungufu wa vyumba vya madarasa katika Mkoa huu wamepanga kujenga maboma ya madarasa 500 ili kukabiliana na tatizo la upungufu katika shule za Msingi katika Mkoa huu kutokana na kasi kubwa ya sasa ya watoto kujiunga na masomo ya shule za Msingi.
Mkoa wa Katavi katika kukabiliana na tatizo la upungufu wa vyumba vya madarasa katika Mkoa huu wamepanga kujenga maboma ya madarasa 500 ili kukabiliana na tatizo la upungufu katika shule za Msingi katika Mkoa huu kutokana na kasi kubwa ya sasa ya watoto kujiunga na masomo ya shule za Msingi.
Hayo
yameelezwa na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko wakati alipokuwa
akiwatubia wajumbe wa kikao 20 wa kamati ya ushauri ya Mkoa wa Katavi
(RCC) kilichofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Mpanda.
Mrindoko amebainisha kuwa kwakutambua hali hiyo Mkoa wa Katavi umejiwekea mkakati wa kuondoa kabisa tatizo la upungufu wa vyumba vya madarasa kwa kuwa na mkakati endelevu na kuweka malengo mbambali mbali kwenye kila Halmashauri ya Mkoa huu.
Baadhi ya wajumbe wa kikao cha kamati ya RCC Wakiwa kwenye ukumbi wa manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi . |
Ametaja mikakati hiyo ni kila Halmashauri wamekubaliana kujenga vyumba vya madarasa mia moja kwa kila Halmashauri ya iliyopo kwenye Halmashauri iliyo kwenye Mkoa huu.
Mrindoko
amefafanua kuwa kutokana na Mkoa kuwa na Halmashauri
tano na kila Halmashauri kwenye mapato yake ya ndani kwa mwaka wa
fedha zimetenga kujenga majengo ya mabomamia moja hivyo kwa mkoa
mzima wanatarajia kujenga maboma 500 ya madarasa .
Amesema
kuwa Mkoa wameisha wasiliana na TAMISEMI ambao wamekubali kutuma pesa ya
maboma yote kwa ajiri ya kukamilisha ujenzi wa madarasa hayo pindi maboma
hayo yatakapokuwa tayari .
Meya wa
Manispaa ya Mpanda Haidari Sumry amesema kuwa Manispaa ya
Mpanda watahakikisha wanatimiza ujenzi wa madoma ya madarasa
waliyopanga kuyajenga kwa mapato yao ya ndani .
Mkuu wa
Wilaya ya Tanganyika Onesmo amewahakikishia wajumbe wa kikao hicho kuwa swala
hilo la ujenzi wa maboma kwenye Halmashauri litatekelezwa kama
ilivyopangwa.