DC: WARYUBA SITAKI WILAYA YENYE MIGOGORO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI

 

Mkuu wa Wilaya ya Malinyi Sebastian Waryuba akizungumnza na wakuu wa Taasisi na vitengo wilayani humo
Na Mwandishi wetu.

Mkuu wa wilaya ya Malinyi Sebastian Waryuba ametoa mwelekeo wake katika utumishi ndani ya wilaya hiyo kwa kusema hataki migogoro ya wakulima na wafugaji.

Wakuu wa Taasisi mbalmbali na Vitengo wakiwa katika kikao kazi kilichoongozwa na Mkuu wa wilaya ya Malinyi Sebastiani Waryuba

Mkuu wa wilaya ya Malinyi Mkoa wa Morogoro Sebastian Waryuba ametoa mwelekeo wake katika utumishi ndani ya wilaya hiyo kwa kusema hataki migogoro ya wakulima na wafugaji.


Akizungumza na wakuu wa taasisi za umma pamoja na wakuu wa divisheni na vitengo katika wilaya hiyo mkuu huyo wa wilaya amesema anajua Kuna migogoro ya wakulima na wafugaji inayoendelea na kuanzia Sasa hataki migogoro hiyo iendelee.

Alisema jambo la kwanza ambalo analifanyia kazi ni kuhakikisha anaondoka migogoro hiyo kwa kukaa na pande hizo kuzungumza nazo na kutatua changamoto zinazowakabili.

Wakuu wa Vitengo Wilaya ya Malinyi wakiwa katika kikao kazi chini ya Mkuu wa Wilaya ya Malinyi Sebastian Waryuba

 "Ugomvi wao  ni wa maslahi ambayo ni ardhi je tutashindwa kutatua?twende na sheria ndogo na kanuni na nitakuja na kanuni ya Malinyi kuhusu migogoro hii naamini tutamaliza tatizo"amesema waryuba

Ameagiza watumishi wote kuliangalia Kwa kina tatizo Hilo la migogoro ya wafugaji na wakulima na kutoa maoni ambayo yatasaidia kumaliza matatizo hayo.

"Nimeambiwa Kuna wafugaji wakorofi 15 ambao wao wanajifanya wapo juu ya sheria Sasa nataka kuonana nao nizingumze nao na tukubaliane namna ya kuishi haiwezekani mkulima akalima mbele ya zizi la mifugo au haiwezekani mfugaji akaingiza mifugo katika shamba la mkulima halafu sisi viongozi tupo"amesema 

Ameagiza kupitia upya mpango wa matumizi Bora ya ardhi ambao utaweza kuonyesha njia sahihi ya kutatua migogoro hiyo.

kwa habari zaidi tembelea ukurasa wetu wa 

kataviclub.blogspot.com

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages