Na Paul Mathias.Katavi
Chama cha Mapinduzi CCM katika mkoa wa Katavi kimeipongeza serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuboresha miundombinu Katika sekta ya Afya kwa vitendo.
Waziri wa Afya Ummy mwalimu katikati mwenye kilemba Cha njano akiwasili katika ofisi za chama cha mapinduzi CCM Mkoa wa Katavi[Picha na Paul Mathias] |
Chama cha Mapinduzi CCM katika mkoa wa Katavi kimeipongeza serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuboresha miundombinu Katika sekta ya Afya kwa vitendo.
‘’lakini tunawatalaamu hapa,tuna mtaalamu wa Masikio pua na
koo bingwa anae bobea Mh waziri hana vifaa tunae daktari bigwa wa Cmt yupo hapa
anapata mshahara lakini tunae daktari wa Bingwa wa hanavitendea kazi sasa ukiwa
na watu wa aina hiyo amamabao ni wasomi katika fani zao wakawa hawako bize
inaleta shida lakini pia hatuna Daktari bingwa wa watoto kwa mkoa wa Katavi
hatuna’’
Katika hatua nyingine Mwenyekiti huyo ameiomba serikali kuaona namna ya kujenga kituo cha kuhifadhia damu katika mkoa wa Katavi ili kupunguza usumbufu kwa wa kupeleka damu katika mkoa wa Tabora ambayo imekuwa chanzo cha vifo kwa wananchi kwa kuchelewa kupata huduma ya Damu.
‘’ukitoka hapa kwenda Mwanza ni kilomita zaidi ya 700 ukitoka
hapa kwenda Rufaa Mbeya ni kilomita 580 utaona nikwanamna gani sisi hapa tulipo
tunamatizo makubwa katika kupata huduma za juu kidogo ombi kwanza umfikishie
Rais ombi la wanakatavi tunamuomba sana Mh Rais atujengee jengo la Damu salama
sasa hivi sasa tukikusanya damu inaenda kusafishwa Mkoa wa Tabora kuna akina
mama wajawazito wakipata kifafa cha Mimba kakma hakuna damu inakuwa tatizo
kwahiyo tunamuomba Rais atusaidie jengo la damu salama’’amesema kimanta
Katika hatua nyingine amesema kujengwa hospitali ya Rufaa
mkoa wa Katavi inakwenda kuwa Mkombozi kwa utoaji wa huduma za matibabu kwa
wanachi wa mkoa wa Katavi.
Kwa upande wake Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema kuwa serikali
imechukua ombi la kujenga kituo cha damu salama katika mkoa wa Katavi pamoja na
mpango wa serikali wa kujenga hospitali ya Kanda mkoa wa Kigoma ili kulahisisha
upatikanaji wa Matibabu kwa wanachi wa mkoa wa Katavi.
Amesema serikali ya mkoa kwa ujumla iendelee kuwatunza
watendaji wa afya kwakuwa wanafanya kazi ya kuokoa uhai wa wananchi pamoja na
changamoto kadhaa zinazo wakabili na serikali ikiwa inaendelea kutatutua
changamoto hizo kwa kadri
inavyowezekakana.
Kwa habari zaidi Tembelea ukurasa wetu wa
kataviclub.blogspot.com