Na Paul mathias ,Mpanda
Halmsahauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi imeweza kutekeleza Mpango wa utoaji wa chakula Shuleni kwa shule za Msingi na Sekondari kwa asilimia 85.3 na kuongeza Chachu ya ufaulu kwa wanafunzi.
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Sophia Kumbuli akizungumnza namana halmashauri yake inavyotekeleza mpango wa chakula Shuleni kwa wanafunzi [Picha na Paul Mathias] |
Kumbuli anasema’suala la Chakula katika Sera ya Elimu
tunalitekeleza katika shule zetu hizi zote ambapo tukifanya shule za msingi na
sekondari tunakuwa na jumla ya shule 68 kati ya hizi shule, shule 58 na kati
yake hapo Shule za msingi 43 na 15 za sekondari zinatoa hicho chakula na hivyo
basi kutupa idadi hiyo ya shule 58 na kuwa na
asilimia 85.3’’
Amebainisha kuwa
wanaendelea na Kampeni ya kuhasisha jamii kupitia kwa wazazi wafahamu umuhimu
wa Mpango wa chakula Shuleni kwa lengo la kutimiza lengo la Asilimia Miamoja
katika kutekeleza mpango huo kwenye manispaa ya Mpanda kwa lengo la kuwa na
ufaulu ubora kwa wanafunzi kwa unaotokana na msukumo wa utoaji wa chakula
Shuleni.
‘’tunafanya hivyo kwa sababu bila chakula inaamaana hakuna
amabae anaweza akafanya masomo kuwa vizuri na hivyo kupitia kutolewa kwa
chakula hawa wazazi amabao jukumu hili liliachwa kwao ikiwa ni pamoja na
chakula na Sare pamoja na Daftari ambalo wanalitimiza kwa kiasi kikubwa
kiukweli basi linapelekea kuinua ufaulu wa shule hizo za msingi na sekondari
kwa mfano shule za Msingi matokeo ya Darasa la Saba yalikuwa asilimia 87 lakini
na sekondari zaidi ya 87 haya yote ni matokeoa ya watoto kupata chakula
shuleni’’
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Sophia Kumbuli akiwa ofisini kwake |
Kuhusu hali ya uripoti wa wanafunzi wa Kidato cha kwanza
2023 hadi sasa kwenye halmsahauri ya Manispaa ya Mpanda umefukia asilimia 92
huku asilimia nane iliyobakia wakiwa wametoa maelekezo kwa watendaji wa kata
na mitaa kupita nyumba kwa nyumba ili kuwabaini wale wote ambao hadi sasa
hawajaripoti shuleni.
‘’nitoe rai kwa watoto kuna asilimia 8 wa shule za sekondari
tuliotegemea ili wafikishe asilimia miamoja ya kuripoti wale form One mpaka
sasa hivi tuna asilimia hiyo 92 na hii asilimia nane tayari jana tumetoa
maelekezo kwa watendaji kuhakikisha wanapita nyumba kwa nyumba kuwaibua hawa
watoto kwenda shuleni “ameeleza Kumbuli
Kila mzazi ana wajibu wa kuhakikisha anaungana na
serikali katika kuunga mkono mipango mbalilimbali katika sekta ya elimu ili
kuimalisha ubora wa Elimu Hapa nchini kwa kutengeneza mazingira wezeshi kwa
watoto ikiwemo kuhakikisha wanakuwa sehemu ya mpango huu wa utaoaji wa chakula
Shuleni.
kwa habari zaidi tembelea ukurasa wetu wa
kataviclub.blogspot.com Endelea kuwa nasi