Mkuregenzi Mkuu wa shirika lisilo la kisrikali la
TAYOBECO Shida Kabulunge akiwatubia wadau
mbambali kabla ya kuzinduliwa kwa mradi wa Boresha Habari
|
Shirika
la lisilo la Kiserikali la Tanzania Behavioural Change Organization
TAYOBECO limezindua Mradi wa Boresha habari wenye lengo la kuhamasisha vijana na
wanawake juu ya umuhimu wa Kupata Chanjo ya UVIKO 19 na chanjo mbalimbali
katika Manispaa ya Mpanda mkoa wa Katavi kwa udhamini wa INTERNEWS ili watu
waweze kuwa na afya Bora.
Baadhi ya washiriki wa Mradi wakiwa katika Picha ya Pamoja |
Mradi
huu umezinduliwa kwenye ukumbi wa Kichangani ulipo kwenye Mtaa wa
Nsemlwa Manispaa ya Mpanda ambao wadau mbalimbali walishiriki kwenye uzinduzi
huu.
Mkurugenzi Mtendajiwa TOYOBECO Shida Kabulunge amesema shirika hilo lisiro la Kiserikali hapa nchi ni lilianzishwa mwaka wa 2019.
Amebainisha
kuwa kutokana na utafiti uliofanywa hivi karibuni imebainika kuwa Mkoa wa
Katavi ni miongoni mwa mikoa mine ambayo imekuwa na mwitikio mdogo kwenye
maswala ya chanjo pamoja na mikoa ya Kigoma ,Njombe na Simiyu hivyo ndio maana
wameona kuna haja ya kutowa elimu kwenye Mkoa wa Katavi .
Shirika hili mwaka 2020/2021 walitowa elimu ya matumizi sahihi ya dawa mpya za kufubaza maambukizi ya UKIMWI Tenofovir,Lamivudine Dolutegravir Ltdkwa Mkoa wa Dar salaam kwa kipindi cha mwaka mmoja na 310 PLHIV walirudi kwenye dawa .
Kabulunge amesema kuwamradi wao watatu wa kutowa elimu ya matumizi salama ya mitandaoni ,ukiwa na lengo la kukomea na kuelimisha jamii juu ya ukatili wa kijinsia mitandaoni ambao ulifadhiliwa na Shirika la Zaina Foundation Tanzania watumiaji 95 mitandaoni waliweza kufikiwa .
Meneja wa programu wa TOYOBECO Adinani
Mussa akielezea namna ya mradi wa Boresha Habari utakavyo
fanya kazi katika Mkoa wa Katavi kwa kuwahamisisha vijana na wanawake juu ya
chanjo ya UVIKO 19 wakati wa uzinduzi wa mradi huu uliofanyika katika ukumbi wa
Kichangani Manispaa ya Mpanda
|
Mradi
huu wa Sai Boresha Habari ulikuwa na malengo
mbambali kiliwemo lengo ambalo wamelizindua kwenye mradi huu katika
Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi .
kwa habari zaidi tembelea ukurasa wetu wa
kataviclub.blogspot.com