Mkuu wa wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph akifunga kikao cha kamati ya ushari DDC Wilaya ya Mpanda |
Na Walter Mguluchuma
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph ameiagiza Mammlaka ya Maji na usafi wa Mazingira Mpanda Muwasa kufatilia kwenye mamlaka zinazo husika ili mradi wa Maji wa Miji 28 katika Bwawa la Milala uanze kutekelezwa ili kutatua kero ya Maji kwa wananchi.
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph ameiagiza Mammlaka ya Maji na usafi wa Mazingira Muwasa kufatilia kwenye mamlaka zinazo husika ili mradi wa Maji wa Miji 28 katika Bwawa la Milala uanze kutekelezwa ili kutatua kero ya Maji kwa wananchi.Viongozi wa serikali na chama Serikali wakiongozwa na Mkuu wa wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph wakiwa katika kikao cha ushauri cha wilaya ya Mpanda DCC
Maagizo hayo ameyatoa wakati akifunga kikao
cha kamti ya ushauri ya Wilaya DCC kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa
Mpanda Social Hall amesema tayari mikataba hiyo imesainiwa na Viongozi wetu wa
juu hivyo nijukumu la mamlaka kufatilia utekelezaji wa Mkataba huo kwani Mji
wetu wa Mpanda nimiongoni wa wanufaika wa mkataba huo kupitia Bwawa la Milala.
‘’mkataba ule uliposainiwa ilitakiwa January
tuanze kuona mkataba ule unatekelezwa kwa hiyo nitumie nafasi hii kuwaagiza
Muwasa habari ya kukaa hapa na kuandika barua na kusubilia wizara si imefanyaje
mfatilie Mradi uanze Mh Rais alishuhudia utiaji saini huo katika mkataba huo wa
miji 28 ikiwemo mji wa Mpanda jukumu letu kama viongozi kumsaidia Rais katika majukumu yetu kwa hiyo Muwasa
mfatilie mradi huu uanze’’amesema Jamila
Watumishi mbalimballi wa halmashauri ya Manispaa ya Mpanda na Halmashauri ya Nsimbo wakiwa katika kikao cha ushauri wilaya ya Mpanda |
‘’janury imeshakatika na sasa tupo
February na inakaribia katikati mkandarasi haonekani eneo la Mradi na hatujui
kitu gani kinaendelea pale kwa hiyo Muwasa mfatilie mradi huo kwa wizara
tunataka mradi unaze kutekelezwa’’
Katika hatua nyingine ameziagiza
Taasisi za serikali kuhakikisha zinapokuwa kwenye vikao mhimu kama DCC kuwa na
taarifa sahihi kwakuwa kikao hicho kina malengo makubwa ya maendeleo ya Wilaya
ya Mpanda.
Viongozi wa dini pamoja na wakuu wa Taasisi wakiwa katika kikao cha ushauri cha Wilaya ya Mpanda. |
Jamila yusuphu amemshukuru Rais wa Jamuhuri
ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuleta fedha
katika sekta ya Elimu ambapo wilaya ya
Mpanda imepokea kiasi cha Shilingi Bilioni 1 na milioni 500 ambazo zimetumika
kujenga Mdarasa 78 kwaajili ya kujenga Madarasa kwa wanafunzi wa kidato cha
kwanza kwa mwaka 2023.
Kwa upande wake Kaimu Katibu Tawala
wilaya ya Mpanda Keneth Pesambili amesema kwa upande wa halamshauri mbili za
Manispaa ya Mpanda na Nsimbo kwa taasisi za Tarula,Muwasa na Ruwasa
zimewasilisha mapendekezo ya Bajeti yenye kiasi cha Shilingi Bilioni 64 .1
kwaajili ya bajeti kwa Mwaka 2023/2024.
kwa habari zaidi tembelea ukurasa wetu wa
kataviclub.blogspot.com