VYOMBO VYA HABARI VINA MCHANGO KATIKA UKUAJI WA KISWAHILI



Na Paul Mathias-KTPC Katavi.

Wanafunzi wa Kidato cha Nne Shule ya Sekondari Nsemlwa Manispaa ya Mpanda Mkoa wa katavi wametembelea ofisi za Chama cha waandidhi wa Habari Mkoa wa katavi kwa lengo kujionea namna habari zinavyoandaliwa na kuchakatwa kabla ya kuchapishwa na kurushwa katika vyombo mbalimbali vya habari

Wanafunzi wa shule ya sekondari Nsemlwa wakiwa katika ofisi za chama cha waandishi wa Habari mkoa wa Katavi.

Wanafunzi wa Kidato cha Nne Shule ya Sekondari Nsemlwa Manispaa ya Mpanda Mkoa wa katavi wametembelea ofisi za Chama cha waandidhi wa Habari Mkoa wa katavi kwa lengo kujionea namna habari zinavyoandaliwa na kuchakatwa kabla ya kuchapishwa na kurushwa katika vyombo mbalimbali vya habari.

Wakiwa katika Mafunzo ya ufahamu  na uelewa namna vyombo vya habari vinavyo fanya kazi kwa umma wamesema kuwa kwa namna moja au nyingine wamekuja kwaajili ya kujifunza namna ya habari zinavyo andaliwa kabla ya kuchapishwa na kurushwa katika vyombo vya habari ikiwemo  Redio,Magazeti,Blogs,Television, naTelevion Mtandaoni.

Wanafunzi hao wamesema kuwa wamejifunza juu ya umuhimu wa vyombo vya habari na waandisahi wa habari namna wanavyo ipasha habari jamii kwa kutumia vyombo vyao vya habari.

wanafunzi wa Shule ya Sekondari Nselwa wakiwa na Mwandishi wa Habari Irene Temu wa uhuru Media katavi

Nikuda Mashaka mwanafunzi wa Kidato cha Nne Shule ya Sekondaeri Nsemlwa  amebainisha kuwa amejifunza kuwa vyombo vya habari vinamchango mkubwa katika ukuzaji wa lugha ya Kiswahili kwakuwa vyombo vya habari kupitia waandishi wa habari hutumia lugha ya Kiswahili kwa ufasasaha kwa wananchi.

‘’nimeona umuhimu wa habari  tunapata habari mbalimbali ambazo tulikuwa hatujui tunazipata kupitia waandishi wa habari tunaweza kueneza Kiswahili kwa kutumia vyombo vya habari ‘’amesema Nikuda.

Amesema kuwa katika ulimwengu huu wa Sayansi na Technolojia amejifunza namna ambavyo vyombo vya habari vinakabiliana na maendeleo hayo ya Utandawazi kwa kuendaana na soko na mazingira yaliyopo.

Kwa upande wake Kiliani Jonh Mwanafunzi wa Kidato cha Nne Nsemlwa Sekondari amesema kuwa vyombo vya habari alivyojifunza vinamchango katika ukuaji wa uchumi kupitia habari mbalimbali za kibiashara na masuala ya kiuchumi.

‘’Vyombo vya habari vinaumuhimu kwa sababu vinakuza lugha yetu na vilevile vinaweza kuchochea ukuaji wa uchumi wa Nchi kupitia taarifa mbalimbali za mambo ya kiuchumi’’ amenena Kiliani

Sadiki Donald ambae alikuwa sehemu ya wanafunzi waliofika katika ofisi za chama cha waandishi wa Habari mkoa wa katavi ameeleza kuwa ametambua kuwa jukumu kubwa la vyombo vya habari kuelimisha,Kuasa, na kukosoa pale inapobidi kama kuna mkanganyiko wa Jambo fulani katika jamii  lenye Masilahi kwa umma ili serikali kuchukua hatua za kiuwajibikaji kwenye jambo husika

Wanafunzi wa kidato cha Nne Nsemlwa Sekondari wakipatiwa uelewa juu ya uandishi wa habari
Mwenyekiti wa chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Katavi Walter Mguluchuma amewashukuru wanafunzi hao kwa kufika kwenye ofisi hizo nan a kujengewa uelewa namna vyombo vya habari katika mkoa wa katavi vinavyo fanya kazi ya kuielmisha jamii kwa Masilahi ya Mkoa na taifa kwa ujumla.

Katika hatua nyingine Walter ametoa wito kwa Wanafunzi wa shule nyingine katika mkoa wa Katavi  kuja katika ofisi hizo kwa kuwa miongoni mwao niwana habari wa siku zijazo

kwa habari zaidi tembelea ukurasa wetu wa 

kataviclub.blogspot.com

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages