WANAFUNZI WAIPA HONGERA SERIKALI UJENZI WA SHULE


Muonekano wa Shule ya Sekondari Anna Lupembe katika kijiji cha Mwenge Kata ya Nsimbo halmashauri ya Nsimbo Mkoa wa Katavi ambayo wanafunzi wameishukuru serikali kwa kuwajengea shule hiyo.[Picha na Paul Mathias]

Na Paul Mathias-Nsimbo

Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Anna  Lupembe iliyopo kijiji cha Mwenge Kata ya Nsimbo halmashauri ya Nsimbo Mkoa wa Katavi wameishukuru serikali kwa kuwajengea shule ya sekondari na kuepuka adha ya kusafiri umbali wa kilomita 10  kufuata huduma ya masomo katika shule ya Sekondari Nsimbo.

Wakizungumnza kwa nyakati tofauti na chombo hiki wanafunzi hao wamesema walikuwa wanasafiri umbali wa kilomita Kumi kupata huduma hiyo katika shule ya Sekondari Nsimbo na kufika wakiwa wamechoka lakini kwa kujengewa shule hiyo itawafanya wasome kwa bidi.

‘’tunamshukuru Rais samia kwa kutujengea shule hii sisi kama wasichana tulikuwa tunapata shida ya umbali mrefu kufuata masomo ila kwa sasa tutasoma kwa amani kwa mfano sisi wasichana tulikuwa tunalubuniwa na kusababisha wengine kupata ujauzito na kuacha shule’’ amesema Diana Godfley  mwanafunzi wa kidato cha kwanza shule ya sekondari Anna Lupembe 

Joseph paul mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika shule ya Sekondari Anna Lupembe sekondari ameeleza kuwa uwepo wa shule ya sekondari kijijini kwao nimukombozi kwakuwa msingi wa maendeleo ni Elimu.

'' kwa sisi wavullana unakuta tunakutana na vijana watushawishi tujifiche vichakani pamoja na kuingia katika makundi Mabaya ila kwa sasa tunashukuru serikali kwa kutujengea shulea hii tutasoma kwa bidiii'' 

Wanafunzi wa shule ya Sekondari Anna Lupembe wakiwa katika Picha ya Tabasamu baada ya kufikiwa na waandishi wa Habari Shuleni Hapo.[Picha na Paul Mathias]

Diwani wa kata ya Nsimbo Maiko Kasanga  amesema ujenzi huo umefanyika kwa jitihada za wananchi pamoja na halamashauri na mbunge wa Jimbo la Nsimbo Anna Lupembe kwa lengo la kutoa elimu kwa wanafunzi hao pasipo na usumbufu wowote.

Amefafanua kuwa kwakuwa maelekezo ya serikali katika uimarishaji wa miundombinu ya elimu katika kila kila kata wameanza kutekeleza maono hayo kwa vitendo.

‘’sisi kama watumishi wa wananchi tumeungana kwa pamoja kwa kushirikiana na viongozi wa Halmashauri pamoja na mbunge wetu Anna lupembe kufanikisha ujenzi huu wa sekondari kwakweli tunaishukuru serikali kwa kulisimamia hili kukamilika kwa shule hii imekuwa ahueni maana wanafunzi walikuwa wanafuata masomo yao katika shule za Mtapenda na Magamba kwakweli tumefurahi sana ‘’amesema diwani huyo

Diwani wa Kata ya Nsimbo Maiko Kasanga akiwa katika shule ya Sekondari Lupembe wakati waandishi wa habari walipotembelea shuleni hapo[Picha na Paul Mathias]

Kwa upande wake Mkuu wa shule ya Sekondari Lupembe Mwalimu Ally Kiduda amesema hadi sasa jumla ya wanafunzi 108 wamelipoti kati ya 123  wameanza kupokea wanafunzi wa Kidato cha kwanza shuleni hapo kwa mwaka huu wa 2023 na masomo yakiwa yanaendelea kutolewa.

''wengi walikuwa wanasomea Nsimbo Sekondari na Wengine Mtapenda umbali wa kilomita 10 kutoka hapa kwahiyo ilikuwa ni changamoto kwa wanafunzi kuchoka sana na kuwafanya kuto hitimu masomo yao lakini kwa kujengewa hii shule ya Anna Lupembe imewasaidia sana kupunguza umbali na hata  morali ya  wanafunzi kuja shuleni imekuwa kubwa ndio maana hata ulipoti wetu kati ya wanafunzi 108 wanafunzi 15 tu ndio hawajalipoti'' amesema kiduda

Katika hatua  nyingine amesema juhudi zinazofanywa na serikali katika kuendelea kujenga miundombinu ya Elimu nikiashiria cha kuhakikisha wao kama walimu wanawajibika kuwafindisha watoto wakiwa shuleni hapo kwa nguvu zote.

Shule hiyo ya Sekondari Anna Lupembe imeanza kujengwa kwa nguvu za wanachi kwa kushirikiana na serikali kupitia halmashauri na Huku mbunge wa jimbo hilo Anna Lupembe kupitia mfuko wa jimbo akitoa Milioni 20  pamoja na Mifuko 50 ya Cementi .

Kwa habari zaidi tembelea ukurasa wetu wa 

kataviclub.blogspot.com

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages