Na Paul MathiasWanawake wa Kitongoji cha Namanyere Kata ya Majimoto Halmsahuri ya Mpimbwe mkoa wa Katavi wakichimba Kaburi baada ya wanaume wa Kitongoji hicho kugoma kushiriki zoezi hilo.
Wanaume
wanaoishi katika Kitongoji cha Namanyere Kata ya Maji Moto Wilaya
ya Mlele Mkoa wa Katavi wamesusia kufanya shughuli za mazishi ya watoto wanao
fariki kwenye Kitongoji hicho wakidai idadi ya vifo vya watoto kuwa
imekuwa kubwa na badala yake shughuli hiyo inafanywe na Wanawake .
Wanawake wa kitongoji cha namanyere wakiwa katika zoezi la Mazishi
Wanaume wanaoishi katika Kitongoji cha Namanyere Kata ya Maji Moto Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi wamesusia kufanya shughuli za mazishi ya watoto wanao fariki kwenye Kitongoji hicho wakidai idadi ya vifo vya watoto kuwa imekuwa kubwa na badala yake shughuli hiyo inafanywe na Wanawake
Mmoja wa
wakazi wa Kijiji hicho John Madirisha amesema
kuwa wanaume wa Kitongoji hicho wamesusia kufanya shughuli za
mazishi kutokana kuongezeka kwa idadi ya vifo vya watoto wachanga
hadi miaka miwili .
Amesema
idadi hiyo ya vifo imekuwa kubwa na kuanza kuwatia
hofu juu ya vifo hivyo na kuamini kuwa vifo hivyo vinatokana na nguvu ya
giza .
‘’sisi
tumechoka kuzika kila siku watoto wanakufa na hao wanaowaua ni baadhi ya
wanawake wa kitongoji hiki kwa kisingizio cha Surua wazike wenyewe’’ amesema
madirisha
Nae
Maiko Msanja mkazi wa kitongoji hicho ameeleza kuwa idadi ya vifo
imekuwa ni kubwa kwenye Kitongoji hicho kwani idadi ya watoto wanao
kufa kwa wiki imefikia wan ne hadi watoto watano.
wanawake wa kitongoji cha Namanyere wakiwa katika mazishi |
Amesema
kuwa hapo nyuma kulikuwa na mlipuko wa ugonjwa wa surua lakini hadi
sasa bado vifo vimeendelea kwa hari hiyo wao hawakubaliani vifo hivyo
kutokana ugonjwa wa surua bali kuna ushirikina unao tokana na
unaofanywa na baadhi ya wanawake kwenye Kitongoji hicho kwa kisingizio cha
ugonjwa wa surua kwa hiyo na mazishi wafanye wanawake wenyewe wao wanaume
wamechoka .
Mwenyekiti
wa Kitongoji cha Namanyere Kata ya Maji Moto Teresia Wikula amekiri
kuwa ni kweli wanaume wa Kitongoji hicho wamesusia kufanya shughuli za
mazishi na shughuli hizo kwa sasa zinafanywa na wanawake.
Amebainisha
kuwa kwa wiki wamekuwa wakijikuta wanazika watoto wane mpaka watoto
watano hali ambayo haijawahi kutokea kenye kitongoji hicho.
Amesema mnamo Desemba mwaka jana kulilipuka ugonjwa wa surua katika Kitongoji hicho ambapo hadi sasa bado kuna wimbi la vifo kwenye Kitongoji na yeye haamini kuwa vifo hivyo vinatokana na na imani za kishirikina ila anacho amini ni mripuko wa ugonjwa wa surua.
Amesema maafisa wa afya wamekuwa wakifika Kitongojini hapo na kuwa elimisha wananchi na kutowa chanjo lakini wananchi wamekuwa na mwitikio mdogo.
Mwenyekiti
huyo wa Kijiji ameomba wataalamu wa Afya katika Halmashauri yao ya
Mpimbwe waongeze nguvu katika kukabiliana na ugonjwa huo ambao umechukuwa
muda mrefu sasa.
Kwa habari zaidi tembelea ukurasa wetu wa
kataviclub.blogspot.com