Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya wilaya ya Mlele Teresia Irafay akiwa na Mkuu wa wilaya ya Mlele Majidi Mwanga wakimkabidhi pikipiki Mtendaji wa kata Ilunde Jacksoni Shura |
Halmashauri
ya Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi imekabidhi pikipiki kwa watendaji wote wa
Kata zilizopo katika Halmashauri hiyo zilizotolewa hivi karibuni na serikali
ili kusaidia utendaji kazi kwa watendaji hao katika shughuli zao za kila siku.
Mhe. Majid Mwanga, Mkuu wa wilaya Mlele akijaribia kuwasha pikipiki zilizotolewa na serikali kwa watendaji wa kata wakati wa hafla ya kuwakabidhi iliyofanyika Halmashauri ya wilaya ya Mlele |
Akikabidhi
pikipiki hizo katika Viunga vya ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Mlele Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmshauri hiyo Teresia Irafay amewaasa watendaji hao kutumia
pikipiki hizo kwa lengo lililokusudiwa ambalo ni kuwahudumia wananchi katika
maeneo yao.
Irafay
ameongeza kuwa pikipiki hizo ikawe chachu ya kufanya kazi kwa bidi na kuwafikia
wanachi kwa wakati na kutatua changamoto zinazowakabili ikiwa ni pamoja na
kutoa elimu kuhusu masuala mabalimbali ya kitaifa.
Wakati
wa makabidhiano hayo Mkuu wa Wilaya ya Mlele Majid Mwanga ameshuhudia
makabidhiano hayo yaliyoenda sambamba na watendaji hao kusaini Mkataba ya matumizi
ya pikipiki hizo baina yao na Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya
Mlele.
Nao
baadhi ya Watendaji wa Kata waliopokea Pikipiki hizo wamesema kuwa watazitunza na
kuzitumia kwa malengo yaliyo kusudiwa na wameishukuru serikali kwa kuwatatulia
changamoto hiyo ya usafiri.
Abdala
Saidi Mkuu wa Kituo cha Polisi Wilaya ya Mlele akitoa neno kwenye hafla hiyo
amewaomba watendaji hao kuzingatia sheria za umiliki wa vyombo hivyo kwa kujifunza
Zaidi katika taasisi zinazotoa mafunzo ya udereva na kupata Leseni ili waweze
kutumia vyombo hivyo kwa mujibu wa sheria.
Serikali
ya awamu ya Sita imekuwa ikiendelea kuboresha miundo mbinu ya watumishi hapa
nchini kwa lengo la kuwasaidia kutimiza majukumu yao pasipo na kikwazo
chochote.
Kwa habari zaidi Tembelea ukurasa wetu wa
kataviclub.blogspot.com