Katika kuadhimisha miaka 46 ya kuzaliwa kwa chama cha mapinduzi mwenyekiti wa CCM mkoa wa Katavi Iddy Kimanta amemwagiza mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko kuakikisha barabara ya Karumbi kwenda Kabatini katika kata ya katuma inatengenezwa.
Katika kuadhimisha miaka 46 ya kuzaliwa kwa chama cha mapinduzi mwenyekiti wa CCM mkoa wa Katavi Iddy Kimanta amemwagiza mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko kuakikisha barabara ya Karumbi kwenda Kabatini katika kata ya katuma inatengenezwa.
Katika Mkutano huo Mwenyekiti alilazimika kutoa maagizo Kwa mkuu wa mkoa kwa mara nyingine baada ya kikundi cha upendo kilichopo kijiji cha Karubi katuma kuomba kupatiwa mashine ya kujamua mafuta ambayo wameiomba muda mrefu lakini bado kumekuwa na changamoto akamuagiza Mkuu wa mkoa kuhakikusha wanakikundi hao wanapatiwa mashine haraka iwezekanavyo. Nataka hawa akina mama uwapatie mashine leo leo unafanyaje mimi sijui itakuwaje mimi sielewi chamsingi hawa wanawake wapewa mashine pamoja na mafunzo ya namna ya kuendesha hiyo mashine.
Chief Mallak akitoa hoja ya kujengwa kwa barabara ya Kirubi Kabatini [Picha na Alex Ngereza] |
katika utekelezaji wa ilani mjumbe wa
halmashauri kuu Taifa CCM Mkoa wa Katavi Gilbart Sampa ameeleza kuwa Ilani ya
CCM ndani ya Mkoa wa katavi imetekelezeka kwa kiwango kikubwa upande wa vituo
vya Afya barabara, maji, Elimu na sekta mbalimbali huduma zimewafikia
wananchi na bado cha Mapinduzi kinaendelea na kitaendelea kuisimamia Serikali
ili iendelee kufikishia maendeleo Wananchi.
Katibu wa Chama cha Mapinduzi Mkoa Mwanamasudy Pazi amesema kwa kipindi hiki kifupi chama hicho kimepata mafanikio makubwa kwa kuwaingiza Wanancha wapya kwa mfumo wa kielektroniki ambao ingizo jipya ni zaidi ya Wanachama 2700
Chalres Malack ni mmoja wa viongozi na mkazi wa eneo la kijiji cha Karubi kabatini amekiomba chama cha Mapinduzi kutoa tamko kuhusu barabara yao kutoka na vijiji hivyo kuwa kitovu cha uzalishaji wa zao la Tumbaku ambapo amesema kwa mwaka mzima huingiza zaidi ya bilioni moja na kwa mwaka huu tunaweza kuzalisha zaidi ya hizo kwa hali ulivyoiona ya njia yetu mwenyekiti tunaomba utoe tamko ili na sisi tupate neema ya ilani ya chama chetu.