![]() |
Mkuu wa idara ya Maendeleo ya Jamii halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika mkoa wa Katavi Halima Kitumba akizungumzia mwenendo wa utoaji wa mikipo kwa Vijana [Picha na Paul Mathias] |
Na Paul Mathias-Tanganyika
Halmashauri ya wilaya ya Tanganyika mkoa wa katavi imeanza kutekeleza Mpango wa kutoa vifaa vya kazi kwa vijana kupitia asilimia nne za mapato ya ndani kama sheria inavyo elekeza .
Hayo
yamebainishwa na Halima Kitumba Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii halmashauri
ya Wilaya ya Tanganyika wakati akizungungumnza katika zaiara ya Mjumbe wa
Baraza wa UVCCM Taifa mkoa wa Katavi Mhandisi Debora Joseph alipotembelea ofisi
hiyo ili kujua mwenendo wa utoaji wa mikopo kwa vijana.
Akito
taarifa hiyo Kitumba amesema kuwa wamekuwa wakitoa Mikopo hiyo kwa vijana kwa
kadri ya Mashart yaliyopo huku miongoni mwavijana hao wakiomba vifaa saidizi
vitakavyo saidia kuendesha Miradi yao kwenye baadhi ya maeneo ya halmashauri
hiyo.
‘’hili
suala tuliagizwa kitaifa na mama Samia tangu akiwa makamu wa Rais na
tunalifanyia kazi ukienda Kasekese nina kikundi cha vijana ambacho kina chakata
mafuta ya Alizeti tuliwapa mashine pia ninakikundi kingine ambacho kinachakata
unga wa sembe tuliwapa Mashine’’ amesema Halima
Pamoja
na hayo ameeleza kuwa vijana katika kijiji cha Kasekese wamewezeshwa fedha hizo
za vijana kwa kuanzisha Ghala lakuhifadhia nafaka pamoja na ghala la kuhifadhi
nafaka katika kijij cha Kamsanga .
‘’kuna
mkopo ambao tumewapa mwaka huu wa fedha robo ya kwanza kuna Ghala limejengwa
Kasekese tuna Maghala Kamsanga tunajitahidi lakini wengine wanakuja na wazo
wanakuambia sisi tunafanya biashara ya kukusanya Mazao kama ni Mazao lazima
umpe Cash kwahiyo wanaotaka vifaa huwatuwapa kipaombele’’ ameeleza Kitumba
Amesema
kikwazo kikubwa kwa Vijana imekuwa ni kutolejesha Fedha hizo kwa wakati hali ambayo imekuwa inawapa changamoto
kutoa fedha hizo kutokana na fedha kuoonekana kwenye vikundi hivyo lakini
katika uhalisia fedha hizo hazionekani kwa kutokulejeshwa.
‘sasa
hivi tu jamani naomba msituingilie tunakwenda Mahakamani kwa vijana vijana
wekuwa ni tatizo wamekuwa na tamaa kwa takwumu za sasa hivi kuna milioni 318
zipo kwa vijana tangu mwaka 2009 nasijui nazipata wapi ameeleza afisa huyo’’
Amebainisha
kuwa kwa Robo ya kwanza tayari wametoa Shilingi Milioni 125 kwa vijana kama
sehemu ya Asilimia nne kwa vikundi vya vijana
Masunga Magaka mkazi wa Kapala Msenga ambae ni kijana anasema suala la Mikopo limekuwa likiwapa changamoto kutokana na baadhi ya vijana kuchukua mkopo na kushidwa kurejesha na wao kukosa fursa hiyo.
‘’kila
tunapomba hii mikopo tunaenda tunaambiwa kuna vijana ambao wamekopa ila
hawajarudisha kwa mfano hapa kapala msenga hakuna vijana waliopatiwa mikopo’’
Nae
Aisha Rashi Mkazi wa Kijiji cha Katuma anasema fursa hii ya mikipo kwa vijana
ni nzuri inawakwamua vijana ingawa vijana wamekuwa wakipata changamoto kwenye
miradi wanayo iibua kwenye maeneo yao.
Kwa habari zaidi tembelea ukurasa wetu wa
Kataviclub.blogspot.com