![]() |
Mjumbe wa Baraza kuu la Taifa UVCCM Mkoa wa Katavi Mhandisi Debora Joseph akiwahutubia baraza la umoja wa vijana wilaya ya Tangantika mkoa wa Katavi[Picha na Paul Mathias] |
Vijana katika mkoa wa katavi wameobwa kuwa waaminifu kwa kulejesha Mikopo ya fedha wanazo kopeshwa na halmashauri zao kupitia Asilimia nne kama maelekezo ya Serikali yanavyo elekeza.
![]() |
Wajumbe wa Braza la umoja wa vijana wa chama cha Mapinduzi ccm Wilaya ya Tanganyika mkoa wa Katavi wakiwa katika kikao cha Baraza hilo [Picha na Paul Mathias[ |
Hayo yameelezwa na Mjumbe wa Baraza kuu Taifa UVCCM Kutoka mkoa wa Katavi Mhandisi Debora Joseph wakati akihutubia kikao cha Baraza la umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Tanganyika kilichofanyika katika Kijiji cha Majalila wilaya ya Tanganyika.
Debora amesema kuwa serikali imekuja na mpango wa kuwawezesha vijana mikopo kupitia halmashauri zao kwa asilimia nne ili kuwainua kiuchumi ila kumekuwa na Shida ya urejeshaji wa Mikopo hiyo kwenye halmashauri hali ambayo hupelekea wengine kukosa mikopo hiyo.
‘’suala la mikopo limekuwa suala mtambuka linaumiza kichwa ukija huku upande wa serikali wanakuambia hivi ukija huku upande wetu wa chama tunaambiwa hivi sasa basi mimi nataka niseme hivi vijana wa ccm niwazembe nafasi tunazopewa tunaaminiwa tunazitumia vibaya ndio maana hatuaminiki mikopo tunapewa tunaaminiwa tunafika pale tumevaa kijani zetu tumependeza tunaheshimika haya sasa tumepewa mikopo tukafanye kazi tunapewa hiyo fursa kwenye kulejesha tunasema hali ni mbaya’’ amesema Debora.
Debora amesema kuwa kutokana na
hali hiyo imewalazimu vinaja wengi kukosa fursa ya kupatiwa mikopo kutokana na
vijana kukopa fedha hizo na kushidwa kuludisha hali inayopelekea vijana wengine
kukosa fursa hiyo.
‘’twendeni sasa sisi ambao tupo
sasa hivi tukailudishe ile Imani mtu ukipewa nafasi ndugu zangu tuitumie ile
nafasi vizuri aliekupa nafasi asijute kukupa nafasi mikopo imekuwa na
changamoto mikopo haturejeshi tunapoenda kuchukua ile mikopo tujilidhishe
vijana wenzangu jambo unalotaka kwenda kufanya lipo sahihi litanilipa? ’’
Amesema sasa niwakati wa
kuelezena ukweli kwa Vijana ili kutengeneza kiazazi cha Vijana chenye uchumi
uliosimama bila kuteteleka kwa kufanya kazi kwa bidiii na nidhamu katika katika
kazi za kila siku ili kuendelea kuaminika katika jamii.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa
umoja wa vijana wa chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Tanganyika David Mussolini
katika wilaya ya Tanganyika vijiji tisa vimetenga maeneo ya kilimo kwa ajili ya
vijana na mpaka sasa hivi kuna ekari Zaidi ya 200 zilizotengwa kwaajili ya
kilimo kwa vijana.
‘’Kwa kata ya Mwese tunavijiji vine
vijiji vitatu vimeanza kutenga maeneo,ukienda kijiji cha lugonesi tumebahatuka
kutenga ekali 50 ambazo zipo na mimi kama mwenyekiti wa umoja wa vijana
nimebahatika kwenda kuziona sambamba na hayo kijiji cha mwese kimeweza kutenga
ekali 10 kwaajili ya vijana hapo mimi nimefika na kuziona na kijiji cha Lwega
kimetenga Ekali 20 ambazo zipo’’
Awali kabla ya kuanza kwa baraza
hilo la umoja wa Vijana wa Wilaya ya Tanganyika Mjumbe wa Baraza kuu Taifa wa
UVCCM Mkoa wa katatavi Mhandisi Debora Joseph ametembelea shule ya sekondari ya
Majalila na kupanda miti pamoja na kutembelea Shule ya Sekondari Kakoso na
Kujionea mwenendo wa Ujenzi wa Mradi wa Bweni shuleni hapo.
kwa habari zaidi tembelea ukurasa wetu wa
kataviblogspot.com