![]() |
Moja ya Trasfoma iliyopo Eneo la Mtemi Beda Kata ya Misunkumilo Manispaa ya Mpanda iliyokatwa nyaya zake za shaba na watu wasiofahamika[Picha na Paul Mathias] |
Shirika la umeme Tanzania Tanesco Mkoa wa katavi limesema halitamfumbia macho yeyote atakae bainika kuhujumu Miundo mbinu ya shirika hilo kwa kuharibu miundo mbinu kwa makusudi hali ambayo inayopelekea kukosekana kwa umeme kutokana na uharibifu huo.
Shirika la umeme Tanzania Tanesco Mkoa wa katavi limesema halitamfumbia macho yeyote atakae bainika kuhujumu Miundo mbinu ya shirika hilo kwa kuharibu miundo mbinu kwa makusudi hali ambayo inayopelekea kukosekana kwa umeme kutokana na uharibifu huo.
Amesema
hadi sasa kuna maeneo Tisa ambayo Trasnfoma zake zimehujumiwa kwa kukatawa nyaya
hizo ikiwemo eneo la Mtaa wa Mtemi Beda kata ya Misunkumilo na eneo la Mtaa wa
kapalangawe kata ya Kazima ambalo waharifu hao walishidwa kutekeleza uharifu
huo kwa kukibizwa na wananchi wakati wa Mchana.
Ameeleza
kuwa waharifu hao wamekuwa wakifanya vitendo hivyo vya kuhujumu miundombinu
hiyo kwa kutumia vifaa kama Mapanga kukata nyaya hizo na kuzichukua na
kuzipeleka kusiko julikana
Amesema
wale wote watakaobanika watakamatwa na kuwafikisha
katika vyombo vya sheria pasipokuwa na huruma dhidi yao
‘’na
nisemetu walewote ambao tutawabaini na kuwakamata tutachukua hatua kali za
kisheria na rai yangu kubwa nitoe wito
kwa wananchi walio karibu na maeneo haya wamepewa dhamana ya kulinda
miundombinu kwa kutoa taarifa tanesco au kwa viongozi wao wa Mitaa’’amefafanua
Abeid
Kwa
upande wake Meneja wa Shirika la umeme Tanzania Tanesco Mkoa wa katavi
Seraphine Lyimo akizungumzia mikakati ya shirika hilo juu ya usalama wa miundo
mbinu ya Tanesco mkoa wa Katavi amesema kuwa awali changamoto hiyo ililipotiwa
katika maeneo ya Inyonga walifanya Doria na kufanikiwa kuwakamata na kuwa
fikisha mahakamani.
![]() |
Meneja wa shirika la umeme Tanzania Tanesco Mkoa wa Katavi Mhandisi Seraphine Lyimo wakati akizungumza na mwandishi wa chombo hiki ofisini kwake [Picha na Paul Mathias] |
Lyimo
amesema wimbi la waharifu hao lililoibuka kwa kukata nyaya za shaba kwenye
baadhi ya maeneo ya Trasfoma za shirika hilo na wanaendelea kufanya dolia kwenye
maeneo hayo ikiwamo hiyo waliyoianza kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na
usalama kuwabaini waharifu hao.
Amefafanua
kuwa wataendelea kutoa elimu kwa wanachi katika maeneo mbvalimbali ya mkoa wa
Katavi juu ya umuhimu wa Kutunza miundombinu ya umeme kwenye maeneo yao kwakuwa
serikali inawekeza fedha nyingi kujenga miundombinu ya umeme.
Nao
baadhi ya wananchi wa Mtaa wa Mtemi Beda ambapo Trasfoma ya imehujumiwa
wameiomba serikali kupitia shirika la ume me Tanesco kuendelea kutoa elimu
ikiwemo kuanzisha ulinzi shirikishi na jamii ya maeneo hayo ili kuzuia uhujumu
huo unafanywa na baadhi ya watu wasiokuwa na nia njema na maendeleo ya mkoa wa
Katavi.
kwa habari zaidi tembelea ukurasa wetu wa
Kataviblog.spot.com