Baba halisi wa Kanisa halisi la Mungu Baba Tanzania akiongoza ibaada ya shukrani katika ukumbi wa Mpanda social hall Mpanda mjini. |
Kanisa Halisi la Mungu Baba Tanzania limesema kuwa litaendelea kuhimiza umoja na mshikamano kwa watanzania ili kuyafikia maendeleo ya kweli katika shughuli zao za kila siku
Kanisa Halisi la Mungu Baba Tanzania limesema kuwa litaendelea kuhimiza umoja na mshikamano kwa watanzania ili kuyafikia maendeleo ya kweli katika shughuli zao za kila siku
Hayo yameelezwa na Baba Halisi wa Kanisa Halisi la Mungu
Baba wakati wa ibada ya shukurani kwa kulipokea kanisa iliyofanyika katika
ukumbi wa Mpanda social hall Mpanda Mjini.
Mungu Baba amesema kanisa la halisi la Mungu Baba linawaombea
watanzania wote pamoja na viongozi wa Taifa ili wafanikiwe kuliongoza taifa la
Tanzania katika hali ya umoja mshikamano na upendo wenye Chemu chemu ya Baraka
ya matumaini.
Katika ibaada hiyo ya shukurani mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa
wa Katavi Keneth Pesambili amesema kuwa mkoa wa katavi unatambua mchango wa
viongozi wa dini katika mkoa wa katavi kwakuwa wanahubiri umoja na Amani kwa
waumini wa mkoa wa katavi.
Pesa mbili amekabidhi skabadhi ya Bank ya shilingi Milioni 3
iliyotolewa na mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko kwaajili ya kusaidia
ujenzi wa kanisa hilo.
Kwa upande wake mtekelezaji wa sauti moja halisi kutoka
Kanisa halisi la Mungu Baba amesema kazi
‘’kubwa ya viongozi
wa kanisa hilo nikufundisha maadili mema kwa jamii kama kanisa tunasisitiza
mambo matatu kwanza Amani,upendo uliopitiliza,na uzalishaji wakati mungu Baba
anamuumba Adamu alimpa bustani ya Aden ailime na kuitunza’’
Amesema kuwa kila siku wamekuwa wakifanya Maombi kwaajili ya
kuwaombea wanachi na Viongozi wa Taifa hili la Tanzania.
‘’kila siku sisi tunaanzaga ibaada saa kumi na moja Alfajiri hadi saa kumi na mbili asubuhi vituo vyote Tanzania kwaajili ya kuombea watu wote serikali yote wanachi wote kwa nini Amani ikitokea basi upendo unatokea kwa watu wote’’