[CHAKUHAWATA] YAPATA VIONGOZI WAO MPANDA YAZOA WANACHAMA KUTOKA CWT.

 

Mwenyekiti wa chama cha kulinda na kutetea haki za walimu Tanzania Datus Mwakasanga  akitoa neno la shukurani baada ya kuchaguliwa katika Manispaa ya Mpanda mkoa wa Katavi .
 
Na Walter Mguluchuma.

Chama cha Walimu cha kulinda na Kutetea Haki za Walimu Tanzania  (CHAKUHAWATA) kIlichoanzishwa hivi karibuni  katika Manispaa ya Mpanda  kimepata viongozi wake wapya watao kiongoza chama hicho kuhu kikiwa kimepata idadi kubwa ya wanachama waliokuwa wanachama wa chama cha walimu CWT .

Wajumbe wa chama cha kulinda na kutetea haki za walimu manispaa ya Mpanda wakiwa katika uchaguzi wa viongozi wao

Chama cha Walimu cha kulinda na Kutetea Haki  za  Walimu  Tanzania  (CHAKUHAWATA) kIlichoanzishwa  hivi karibuni  katika Manispaa ya Mpanda  kimepata viongozi wake wapya watao kiongoza chama hicho kuhu kikiwa kimepata idadi kubwa ya wanachama waliokuwa wanachama wa chama cha walimu CWT 

Kati ya idadi ya walimu   891 waliopo katika shule  za Msingi na Sekondari  CHAKUHAWATA  kimeweza kufanikiwa kwa kipindi hiki kifupi kuwa na idadi ya wanachama 632 ambao ni sawa na asilimia 90 ya walimu  wote waliopo katika Manispaa ya Mpanda .

 Viongozi wa chama hicho  waliochaguliwa kwenye mkutano mkuu wa Chama hicho uliofanyika katika ukumbi wa CCM  Wilaya ya  Mpanda  nafasi ya  Mwenyekiti wa  Chama cha  CHAKUHAWATA Wilaya ya Mpanda ni  Datus  Mwakasanga   alipata kura 26 dhidi ya  Benjamini  Masai  aliyepata kura 25 ,katibu amechaguliwa  kuwa ni  Nyavidunda  Mhule .

Benjamini Masai Mgombea akiomba kura kwa wajumbe kwa unyenyekevu lakini katika uchaguzi huo kura hazikutosha za kuwa mwenyekiti wa chama hicho.

Viongozi wengine waliochaguliwa nafasi ya mhasibu ni  Nahorry  Sanga ,mwakilishi wa wanawake  Vumilia  Ndazi ,mwakilishi wa  vikao vya Taifa  Slingwa Masoto  na mwakilishi wa watu wenye ulemavu amechaguliwa  Obed Malenga .

 Akisoma taarifa  ya chama hicho kabla ya kuanza kwa uchaguzi aliyekuwa kaimu Katibu  Chakuhawata  Nyavidunda  Mhule  Wilaya  ya Mpanda  alisema kuwa  chama hicho katika Wilaya ya Mpanda  kilianza mwaka  2021 kikiwa na mwanachama mmoja  hadi sasa kina wanachama 632 kati ya wanachama  891 walipo katika Manispaa ya Mpanda .

Amebainisha kuwa  chama hicho kimekuwa na mafanikio  ikiwa ni pamoja na kongeza wanachama kwa idadi kubwa ,kutowa elimu kwa wanachama  kuhusu uwajibikaji  kutowa namna bora juu ya kudai haki .

Safu ya uongozi Mpya wa Chama cha Kulinda na kutetea Haki za Tanzania Katika manispaa ya Mpanda baada ya kuchaguliwa.

Pia elimu kuhusu  miiko  ya  taaluma  ya ualimu  kuwaondolea  wanachama  makato ya asilimia mbili  iliyokuwa inakatwa kwenye mishahara  yao kama ada  ya  uanachama  na badala yake kwenye chama hicho  itakuwa   ni  makato ya shilingi elfu tano tuu na sio kama walivyokuwa wakikatwa asilimia mbili ya mshahara .

 Katibu  msaidizi  tume  ya utumishi wa  walimu  amesema   viongozi wasifurahie kuchaguliwa bali wahakikishe wanaisaidia  tume ya utumishi wa walimukutatua migogoro  ya walimu  na pia watowe huduma bora kwa wanachama wao .

 Amewaonya  kutojihusisha na malumbano na chama kingine cha Walimu  cha  CWT     na badala yake wanatakiwa kuhakikisha wanafanya kazi ya kukijenga chama  chao kwa masilahi mapana ya wanachama wao 

Kwa upande wake  mdhibiti wa ubora  elimu wa Manispaa ya Mpanda  Leonald  Simbeye  amesema kuwa  chama hicho kinatakiwa kufanya kazi zake kwa kuzingatia  katiba yao na si kufanya kazi za kupingana na Serikali.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages