Mratibu wa Mradi wa PETS kutoka shirika la Grean Leaf akitoa taarifa ya mwenendo wa mradi katika halmashauri ya Nsimbo. |
Shirika la Grean Leaf Tanzania inayotekeleza Mradi wa kuwajengea uwezo wananchi kuhusu ufatiliaji wa matumizi ya fedha za umma katika miradi ya elimu ya Msingi Katika halmashauri ya Nsimbo Mkoa wa Katavi imesema wananchi wamekuwa na uelewa juu ya Ushilikishwaji na ushiriki wa jamii wa matumizi ya fedha za umma zinazoletwa na Serikali .
Hayo yamebainishwa na Mratibu
wa huo mradi Anord Lumbi wakati wa kikao cha Mrejesho kamati za PETS Katika
maeneo ya Mradi unapotekelezwa katika kata za Kanoge,Katumba,Kapalala na
Nsimbo.
Anord amebainisha kuwa Mradi
huo unatekelezwa na Taasisi ya Green Leaf Organization kwa ufadhili wa Shirika
la Foundation for civil society wenye Gharama ya shilingi million 39 ambapo
jumla ya shule nane za msingi katika kata hizo zitanufaika na mradi huo.
Joyce Benedictor Mwenyekiti wa Kamati ya Pets akitoa taarifa ya Mrejesho kwa kazi iliyofanywa na kamati hiyo katika maeneo ya mradi wa Pets katika kata nne za Halmashauri ya Nsimbo. |
Awali akiwasilisha taarifa ya
Mrejesho wa [PETS] kwa kata zinazonufaika na mradi huo Joyce Benedictor amebainisha
kuwa kamati hizo zimebaini baadhi ya changamoto ikiwemo Mrundikano wa Wanafunzi
kwa baadhi ya shule,Miundombinu kutokuwa toshelevu,Uchakavu kwa baadhi ya
Majengo ya shule pamoja na Rasilimali
watu kuwa chache kwenye baadhi ya shule.
Ameishauri serikali kuendelea
kuzitatua kero hizo kwa kadri inavyowezekana ili kuhakikisha watoto wanapata
elimu katika mazingira salama.
Katika hatua nyingine
ameipongeza serikali kwa kuendelea kutatua changamoto ya miundombinu kwa ujenzi
wa Madarasa na Mabweni kwa wanafunzi.
Baadhi ya Madiwani walioshiriki katika kikao cha Mrejesho wa kamati za Pets wakiwa na kaimu mkurugenzi Halmashauri ya Nsimbo Erimkwasi Jonh[ wa Tatu toka kushoto] |
‘’wananchi kupitia kamati hizi
za PETS wananchi wameamka wameweza kufatilia matumizi ya fedha za umma katika
shule zetu hizi kwa ukaribu sana imewafanya hata waalimu katika shughuli zinazo
husu fedha kuziweka wazi katika mbao za matangazo amesema Erimkwasi’’
Amebainisha kazi mbalimbali
zinazo husu ujenzi kwa kuwapata mafundi umekuwa shirikishi kwa kufuata kanuni
na taratibu kwa uwazi zaidi hii inatokana na kamati hizi za PETS kusimamia
uwajibikaji.
Diwani wa Kata ya Katumba Rajab Said akizumgumzia namna Mradi wa Pets unavyotekelezwa katika kata ya Katumba. |
Diwani wa kata ya Kanoge Salehe Mrisho na diwani wa Kata ya Katumba Rajabu Said wamebainisha kuwa Grean Leaf kupitia Mradi wa PETS umeawasadia madiwani kuweza kufatilia kwa kina matumizi ya fedha zinazoletwa na serikali kwenye kata zao.