Moja ya bidhaa zinazopatikana katika soko la Mitumba eneo la Kituo cha zamani cha Mabasi maalufu Stand ya zamani Mpanda Mjini |
Na Paul mathias Katavi.
Wafanyabiashara wa Mitumba Eneo la Stand ya Zamani Halmshauri ya Manispaa ya Mpanda mkoa wa Katavi wameiomba serikali kuendelea kuboresha Miundo mbinu ya soko hilo ikiwemo Maji,Taa.
Wafanyabiashara wa Mitumba Eneo la Stand ya Zamani Halmshauri ya Manispaa ya Mpanda mkoa wa Katavi wameiomba serikali kuendelea kuboresha Miundo mbinu ya soko hilo ikiwemo Maji,Taa ,na kumwaga Vifusi kwenye maeneo yanayoonekana kuwa na Mabonde mabonde.Baadhi ya wafanya biashara katika soko la mitumba eneo la stand ya zamani wakiwa katika kazi zao za kila siku.
Wamebainisha kuwa
hali hiyo imekuwa ikiwapa shida na kuingia gharama ya kununua maji shilingi 250
kwa dumu moja kwaajili ya matumizi mengine ya kawaida sokoni hapo.
‘’Inatulazimu
kununua maji kwa sababu yaliyopo nikwaajili ya huduma ya choo hali ambayo
kiafya huwezi kuyatumia ikizingatiwa Tank la Maji lipo Karibu na Choo ‘’amesema
mmoja wa wafanyabiashara hao sokoni hapo.
Wamesema kutokana
na Shughuli kuendelea kufanyika hadi nyakati za usiku wanaomba mamlaka zinazo
husika kuwafungia Taa za kisasa ili kuendelea kufanya kazi zao hadi
nyakati za usiku tofauti na sasa ambapo huwalazimu kufunga Mapema.
Katika hatua
nyingine wameishukuru halmashauri ya Manispaa ya Mpanda kwa kufanya maamuzi ya
kuziruhusu Gari ziendazo Vijijini Kuegesha hapo hali ambayo imeongeza mara dufu
wateja wa biashara zao husususani Nguo,Vyakula na usafiri wa Boda boda kupata
wateja.
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Sophia Kumbuli akizungumzia mikakati ya kuendelea kuboresha miundo mbinu ya soko la mitumba Stand ya zamani. |
Maria Jonh
Mamalishe katika soko hilo amesema ‘’mimi nimekuwa hapa kwa muda mrefu zamani
tulikuwa tunalaza vyakula kwa kukosa wateja ila leo tunashukuru baada ya Magari
haya kutoka vijijijini kuruhusiwa kufanya maegesho hapa tunapata wateja’’
Mwenyekiti wa Soko
hilo Jofley Tendesigulu ameishukuru halmashauri kwa kuona umuhimu wa kuipa uhai
Stand ya Zamani kwa Magari ya vijijini kuegesha katika eneo hilo hali ambayo
imeongeza wateja katika Biashara zao.
Moja ya mama lishe katika eneo la stand ya zamani akiwa katika kazi zake |
‘’tunamia Maji ambayo yanatoka maeneo ya chooni kule kuna bomba ambalolinafunguliwa kwenye eneo la choo ingawa wengi hawatumiii katika matumizi ya kawaida na tayari tumeandika barua kwa mkurugenzi wa Manispaa ya kuwaomba Muwasa watufungie Gati kwaajili ya matumizi memngine ya Maji sokoni hapo ‘