Walter Mguluchuma na Paul Mathias Katavi.
Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Katavi (KRFA) kimeshaurikushirikisha wadau mbambali wa michezo waliko mkoani hapa nan je ya Mkoa ikiwa ni katika jitihada za kuinua soka la Mkoa huu na kuendeleza vipaji kwa vijana.
Chama
cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Katavi (KRFA)
kimeshaurikushirikisha wadau mbambali wa michezo waliko mkoani hapa
nan je ya Mkoa ikiwa ni katika jitihada za kuinua soka la Mkoa huu
na kuendeleza vipaji kwa vijana .
Ushauri
huu umetolewa katika ufunguzi wa Mkutano mkuu wa chama
hicho uliofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Mpanda na mgeni
rasmi wa mkutano huo Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa
wa Katavi Idd Hassan Kimanta( Mkuu wa Mkoa Mstaafu) kwenye
hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano .
Amesema kuwa mkoa wa Katavi kuna vipaji vikubwa sana vya vijana wanao jua kucheza mpira isipokuwa bado hawaja shirikishwa inavyotakiwa kwa kuwakusanya vijana wa kutoka maeneo mbambambali kama vile ya mwambao mwa ziwa Tanganyia na kuwaandalia mashindano mbambambali ya kuanzia ngazi ya Kata na kuendelea.
Kimanta
ameshauri kuwa ili kuweza kuendeleza soka kwa Mkoa wa Katavi ni lazima
KRFA iwashirikishe wadau mbali mbali wa soka wa ndani ya Mkoa
huu na wale wan je ya Mkoa wa Katavi
Amesema
kuwa watu wacheze mpira wasishindwe kucheza mpira kwa kisingizio
cha viwanja kwani viwanja vipo watumie hata viwanja vya shule za msingi
pindi wanafunzi watakapo kuwa wametoka shuleni .
Amebainisha
kuwa hakuna kitu kigumu kama kuendesha timu kwa sababu wachezaji wanapaswa
kutuzwa sasa unawatunzaje pia wanahitaji vifaa vya mpira mfano mpira
mmoja mzuri ni laki mbili na nusu hivyo bila kuwa na wadau timu haiwezi
kuumudu gharama ya kuendesha timu .
Mwenyekiti
wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Katavi Keneth Pesambili amesema chama hicho
kinapata changamoto kubwa ya timu inapokuwa imepata nafasi ya kuwakilisha
Mkoa kwenye mashindano kama ya mabingwa wa mikoa jukumu hilo la
timu limekuwa ni kama la chama cha soka cha mpira wa miguu Mkoa wa
Katavi hiyo ni kutokana na vilabu husika kutokuwa na ufadhili
..
Amesema
kama timu zitapata udhamini kuna uhakika wa timu za kutoka Mkoa wa
Katavi zikawa zinafanya vizuri kama ambavyo ilivyokuwa timu ya
Katavi Renger iliyokuwa ikimilikiwa na Halmashauri.
Amevitaka
vyama vya mpira wa miguu vya kwenye Wilaya hiyo kuhakikisha ligi ya ngazi
ya Wilaya inachezwa kwenye kila Wilaya ili mpira uchezwe kwenye maeneo yote
kuliko ilivyo sasa ambapo kuna Wilaya zimekuwa hazifanyi mashindano ya ligi
kwenye ngazi zao .
Pesembili
amewaambia wajumbe wa mkutano huo mkuu wa KRFA kuwa wao wamekuwa
wakihakisha kila mwaka wanafanya mashindano yote ya kuanzia mashindano ya
vijana na mashindano mengine yote ambayo yapo kwa mujibu TFF.