![]() |
Mbunge wa Viti maalumu Mkoa wa Katavi,Tusker Mbogo akizungumnza wakati wa kukabidhi Pikipiki nne kwa Jumuiya ya wanawake wa chama cha Mapinduzi CCM mkoa wa Katavi. |
Mbunge
wa Viti Maalumu katika mkoa wa Katavi Tusker Mbogo ametoa Pikipiki nne Zenye
zaidi ya Milioni 10 kwa Jumuiya Umoja wa wanawake wa chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Katavi kwa lengo la kujiimalisha
kiuchumi.
![]() |
Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi CCM mkoa wa katavi Iddi Kimanta akipokea vielelezo vya Pikipiki kutoka Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa katavi Tusker Mbogo. |
Mbunge wa Viti Maalumu katika mkoa wa Katavi Tusker Mbogo ametoa Pikipiki nne Zenye zaidi ya Milion 10 kwa Jumuiya Umoja wa wanawake wa chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Katavi kwa lengo la kujiimalisha kiuchumi.
Ajkizungumnza katika hafla ya kukabidhi Pikipiki hizo iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano katika Ofisi za Chama cha Mpainduzi Wilaya ya Mpanda mbele ya Mgeni Rasimi katika shuhguli hiyo Mwenyekiti wa chama cha Mpanduzi Mkoa wa Katavi Iddy Kimanta.
Tusker
amesema kuwa kwa kutambua mchango unaotolewa na Jumuiya ya umoja wa wanawake wa
chama cha Mapinduzi CC Mkoa wa Katavi UWT amewiwa kutoa pikipiki hizo ili
zisaidie katika kuimalisha uchumi wa jumuiya hiyo ndani ya chama cha mapinduzi
mkoa wa Katavi.
‘’Nimeona
ni wajibu wangu kama mbunge wa viti maalumu wa mkoa wa Katavi kutoa pikipiki
hizi ambazo zitakuwa kama mradi wa bodaboda ili uweze kuiendeleza jumuiya ya
UWT na akina mama wa chama cha Mapinduzi mkoa wa Katavi amesema “Tusker
“Lakini
pia tunapokwenda kwenye uchaguzi w serikali za mitaa iliiakina mama hawa waweze
kufanya kampeni Vizuri lakini tunapo kwenda katika uchaguzi wa 2025 wasije
kusema tumekosa usafiri katika utekelezaji wa majukumu yao katika nyakati hizo
za uchaguzi”
Kuhusu
kazi zinazofanywa na serikali ya awamu ya Sita Chini ya Rais Dk Samia Suluhu
Hassan Tusker Mbogo amesema kumeshuhudiwa maendeleo katika sekta za
Barabara,Maji,Afya,Elimu pamoja na mageuzi mbalimbali katika sekta za nishati
na uwekezaji katika mkoa wa Katavi tofauti na miaka mingi ilivyokuwa.
Mwenyekiti
wa chama cha Mapinduzi CCM mkoa wa Katavi Iddy Kimanta amesema msingi wa chama
cha mapinduzi ni kusimamia Vitega uchumi vilivyopo ndani ya chama cha mapinduzi
mkoa wa Katavi na hatomuonea mtu ambaye anahujumu kulipa mapato yanayotokana na
vyanzo mapato ndani ya chama hususani Vibanda.
![]() |
Baadhi ya wanawake wa UWT mkoa wa katavi wakiwa katika hafla ya kukabidhiwa pikipiki |
Katika
hatua nnyingine amemshukuru Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Katavi kwa kutoa
pikipiki hizo ambazo zitaisadia jumuiya ya UWT Kujiendesha kichumi hali
itayosaidia chama cha mapinduzi kuendelea kuwaimala zaidi.
Mwenyekiti
wa UWT mkoa wa Katavi Fortunatus Kabeja awali akitoa salamu kwa niaba ya
jumuiya hiyo amesema jamii lazima iendelee kuwalea watoto katika misingi ya
maadili ya kitanzania na kuepuka tabia za kufuata mikumbo na kuiga tamaduni za
kigeni.
![]() |
wanachama wa chama cha Mapinduzi CCM mkoa wa katavi wakiongozwa na mwenyekiti wa chama hicho Iddi Kimanta katika |
“Sisi
kama wanawake tukatae ukatili wa kijinsia kwa watoto wetu na tuwalee katika
maadili na misingi ya kitanzania ili kuendelea kuwa kizazi chenye maadili
kwenye jamii”
Pikipiki hizo zilizotolewa na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Katavi Tusker Mbogo zimeakabidhiwa kwa mwenyekiti wa CCM mkoa wa Katavi na kugawiwa kwa Makatibu wa UWT katika wilaya za Mpanda, Mlele, Tanganyika, Huku chama cha Mapinduzi CCM mkoa kikipatiwa pikipiki moja.