Na Paul mathias-Katavi
Serikali katika mkoa wa Katavi imesema
inatambua mchango unaotolewa na sekta ya madini kwa kuchangia pato la serikali
na kukuza uchumi wa mkoa wa Katavi.
Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko [wanne kutoka kulia] akiwa katika ziara ya kutembelea maeneo ya uchimbaji wa madini katika mgodi wa madini wa Katavi Mining. |
‘’tulipoanza soko hili mwaka 2019 dhahabu
ambayo ilikuwa inauzwa wakati huo ilikuwa ni 801 .5 Gram ambazo thamani yake ni
kama Milioni 62 lakini mpaka sasa tunavyozungumnza tulipo hapa march 2023
tayari kwa kutumia soko hili mkoa umeweza kukusanya dhahabu Tani 1.185 kwa
maana ya kilo milioni moja lakimoja na semanini na tano elf mia saba semanini
na sita zenye thamani ya Bilioni 130.1
hayo ni mafanikio makubwa katika sekta ya madini’’amesema mrindoko
Akiwa katika soko hilo la madini mkoa wa Katavi
Mrindoko amesema serikali itaendelea kuimalisha miundombinu katika sekta ya
madini ili serikali iendelee kupata mapato kupitia madini.
Mohamed Abdullazak Mwekezaji wa Mgodi wa Katavi Mining [wa kwanza kulia] akitoa maelezo kwa mkuu wa mkoa wa katavi Mwanamvua Mrindoko baada ya kutembelea mgodi huo. |
Twaribu Serf Meneja wa Katavi Mining amesema
changamoto ya uendeshaji wa Mgodi huo kwa kutegemea umeme wa mafuta umekuwa
ukiwa gharimu na kuiomba serikali pindi umeme wa Grid ya Taifa ya umeme utakapo
fika katika mkoa wa Katavi Mgodi huo upewa kipaombele ili kupunguza gharama za
uendeshaji kwa kutegemea umeme wamafuta ya Disel.
Sehemu ya mitambo inayotumika katika shughuli mbambali kwenye Mgodi wa Madini wa katavi Mining. |