TANROADS KUTUMIA BIL 21 KWA MATENGENEZO YA BARABARA KATAVI.


Meneja wa TANROADS Mkoa wa Katavi Mhandisi Martini Mwakabende akiwasilisha Rasimu ya Bajeti ya Tanroads Mkoa wa Katavi kwa Mwaka 2023/2024[Picha na Paul Mathias]

Na Walter Mguluchuma, Katavi.

Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS)  Mkoa wa Katavi  imepanga kutumia kiasi cha  Zaidi ya Tshs  Bilioni 21 kwaajiri ya matengenezo ya barabara kwa ajiri yam waka wa fedha 2023/2024 huku Zaidi ya   Tshs  Bilioni 10 zikiwa  ni  kutoka  mfuko  wa Barabara.

Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Mwanamvua Mrindoko akifungua kikao cha bodi ya barabara kilichofanyika leo katika ukumbi wa manispaa ya Mpanda.- (Na picha na Paul Mathias)
Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS)  Mkoa wa Katavi  imepanga kutumia kiasi cha  Zaidi ya Tshs  Bilioni 21 kwaajiri ya matengenezo ya barabara kwa ajiri yam waka wa fedha 2023/2024 huku Zaidi ya   Tshs  Bilioni 10 zikiwa  ni  kutoka  mfuko  wa Barabara

 Hayo yamesemwa na Meneja wa Taroads Mkoa wa Katavi  Mwandisi Martin Mwakabende wakati alipokuwa akiwasilisha rasimu ya bajeti ya Taroads Mkoa wa Katavi yam waka wa fedha  2023/2024  kwenye  kikao cha 20  cha  Bodi ya barabara  ya Barara ya Mkoa wa Katavi kilichofanyika katika   ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda .

Mwakabende ameeleza kuwa  kwa mwaka ujao wa fedha  wameomba kuizinishiwa bajeti ya  kiasi cha Tshs Bilioni  21. 885 kati ya fedha hizo Tshs  10,581,392 fedha za  kutoka mfuko wa barabara  na kiasi cha  Tshs Bilioni 11, 304,600,000 ni za kutoka  mfuko wa Maendeleo .

Amesema  katika mwaka wa fedha  2022/2023 walitengewa kiasi cha Tshs Bilioni 17.2 kwa  ajiri ya kufanyia matengenezo barabara  na ukarabati  na hadi kufikia  tarehe 28/2/ 2023  walikuwa wamepokea kiasi cha  Tshs Bilioni  7.1 ambazo ni sawa na asilimia  55. 98 ya bajeti ya matengenezo ya barabara

Amebainisha kuwa   TANROADS  Mkoa wa Katavi  wameendelea  kuthibiti  magari mazito  kwa  kuyapima  na mizigo na yakibainika  yamezidisha  uzito hutozwa  gharama  za uharibifu  kwa mujibu wa sheria  ya usalama  Barabarani  yam waka ( Road Trafffic Act)  1973 kwa lengo  la kutunza  usalama  na  kudhibiti uzito wa magari barabarani .

Mwakabende amezitaja  changamoto  zilizopo kwenye utekelezaji  wa kazi zao kuwa ni  wananchi  kupitisha mifugo yao  barabarani  na hivyo  kuchangia  kwa kiasi kikubwa  uharibifu wa  barabara , wananchi kufanya  shughuli za kilimo  ndani  ya maeneo  ya Hifadhi  ya Barabara  kama ya Kagwila kwenda Karema.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi Ali Makame Hamadi akichangia hoja katika kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Katavi[Picha na Paul Mathias]

Pia  fedha zinazotolewa  kwa ajiri  ya miradi ya maendeleo  kutokidhi  mahitaji halisi  ya ukarabati wa barabara  na  uharibifu  wa alama za  usalama barabarani  kunaongeza  gharama  za matengenezo  ya barabara  na kuhatarisha usalama wa watumiaji wa  barabara.

Mbunge wa Jimbo  la  Mpanda  Sebastian Kapufi aliomba  Taroads kuwalipa haraka wananchi fidia zao waliopisha ujenzi wa barabara za Mpanda Sitalike na Mpanda  Ugalla  ambao wanamuda mrefu sasa hawaja lipwa fidia zao .

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlele Sudi Mbogo  amewapongeza Taroads Mkoa wa Katavi kwa kazi nzuri wanayofanya  ya ujenzi wa barabara na kuzisimamia vizuri  hali ambayo imefanya  ulahisishaji wa usafiri .

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko  alisema ni kweli kuna changamoto ya watu kuharibu miundo mbinu ya barabara hivyo ameliagiza jeshi la polisi kuwasaka na kuwakamata watu wote wanaofanya uharibifu huo na kwa wale watao bainika kununua miundo mbinu hiyo kama vyuma chakavu hata sita mara moja kuwachukulia hatua .

Ameshauri elimu ya utunzaji wa barabara kwa wananchi iendelee kutolewa   kwani ni muhimu wananchi kuelewa umuhimu wa   barabara zinapo kuwa zinapita kwenye maeneo yao .

Rc Mrindoko kuhusu fidia za wananchi wanao dai amesema kuwa  Serikali kweli inatambua  kuwa wananchi hao wanadai fidia na ipo katika hatua mbambali juu ya utekelezaji wa swala hilo .

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages