Mbunge wa Jimbo la Mpanda Mjini Mkoa wa Katavi,Sebastian Kapufi akichangia hoja zilizoibuka kwenye kikao cha bodi ya barabara Mkoa wa Katavi- (Na Picha na George Mwigulu) |
Na Walter Mguluchuma, Katavi
Mbunge wa Jimbo la Mpanda Mjini ameomba wananchi waliopisha ujenzi wa Barabara za kiwango cha lami za Mpanda Sitalike na Kawajense kwenda Ugalla walipwe fidia zao wanazodai kwa muda mrefu sasa.
Meneja wa TANROADS Mkoa wa Katavi,Mhadisi Martin Mwakabende akitoa ufafanuzi wa masuala mbali mbali ya barabara kwenye kikao cha bodi ya barabara mkoa wa Katavi- (Na Picha Paul Mathias) |
Mbunge wa Jimbo la Mpanda Mjini ameomba wananchi waliopisha ujenzi wa Barabara za kiwango cha lami za Mpanda Sitalike na Kawajense kwenda Ugalla walipwe fidia zao wanazodai kwa muda mrefu sasa .
Kapufi ametowa kilio cha wananchi hao wakati wa kikao cha bodi
ya barabara cha Mkoa wa Katavi kilichofanyika katika ukumbi wa
Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda kilichoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa
Katavi Mwanamvua Mrindoko .
Amebainisha kuwa kuna wananchi wamepisha ujenzi wa
barabara za kiwango cha Lami kutoka Mpanda kwenda Sitalike na Kawajense kwenda
Ugalla wanadai fedha zao kwa muda mrefu sasa nab ado hawaja lipwa fidia
zao hizo .
Amesema hali hiyo inawafanya wananchi waliopisha ujenzi huo
kuanguka kiuchumi kwani nyumba zao zimepigwa alama ya x ambayo inaamanisha kuwa
wanatakiwa walipwe fidia zao kama ambavyo walivyofanyiwa tathimini
ya gharama za nyumba zao .
Kapufi amefafanua kuwa wananchi hao baada ya kuwa
wamewekewa wameshindwa kuendeleza majengo mengine ya nyumba
na wao wametii maelekezo hayo kwanini sasa wao wanao washindwe
kulipwa fidia zao .
Meneja wa Taroads Mkoa wa Katavi Mwandisi Martin
Mwakabende ameeleza kuwa swala la wananchi hao tayari lipo kwenye ngazi ya
Wizara huku Mkoani wao wameisha tekeleza yale waliopaswa kufanya .
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko amesema kuwa swala la wananchi hao juu ya madai yao ya fidia Serikali inalitambua na wanafahamu wanaichi hao wana dai fidia kwa ajiri ya kupisha ujenzi wa barabara za kiwango cha lami.