AFARIKI KWA KUANGUKIWA NA NYUMBA.


Muonekano wa Nyumba ya Khadija Eneriko iliyopo Mtaa wa Shanwe ambayo imebomoka na kusabisha kifo cha Elizabeth Fabiano usiku walipokuwa wamelala

Na Paul Mthias -Katavi.

Mkazi mmoja wa Mtaa wa Shanwe Manispaa ya Mpanda mkoa wa Katavi amefariki dunia baada ya kuangukiwa na nyumba usiku alipokuwa amelala.

Khadija Eneriko Mkazi wa Mtaa wa Shanwe aliyepoteza Mtoto wake kwa kuangukiwa na nyumba 
Mkazi mmoja wa Mtaa wa Shanwe Manispaa ya Mpanda mkoa wa Katavi amefariki dunia baada ya kuangukiwa na nyumba usiku alipokuwa amelala.

Akizungumzia tukio hilo mama mzazi wa Marehemu Khadija Eneliko amesema mtoto wake Elizabeth Fabiano amekutwa na madhila ya kifo hicho usiku wa kuamkia Jumapili ya 16/4/2023 walipokuwa wamelala kwenye nyumba hiyo.

,,tulipokuwa tumelala kidogo usiku tukasikia Mvua inanyesha na baada ya muda kidogo tukasikia ukuta wa nyumba unaanguka kwa nguvu na hapo mwanangu ukuta ukamdondokea sehemu ya Mgongo na maeneo mengine ya mwili ‘’amesema Khadija

Ameeleza kuwa baada ya hapo aliomba msaada kwa majirani na walimpeleka hospital lakini akiwa anapatiwa matibabu alifariki Dunia

Rehema juma mkazi wa Mtaa wa shanwe amesema kuwa Marehemu alikuwa anaishi na jamii katika mwenendo uliomwema na wamesikitika kwa janga hilo ambalo limepelekea kupoteza uhai wake.

‘’Tunaomba serikali iweze kuangalia uwezekano wa kumjengea nyumba nyingine Bibi huyu kwani hapa alipo mazingira siyo salama nyumba bado inaonekana kuwa na mipasuko mipasuko lolote la weza kutokea ,,

Waombolezaji wakiwa katika Msiba wa Elizabeth Fabiano alefariki kwa kuangukiwa na Nyumba Mtaa wa Shanwe.
Katika hatua nyingine Rais Msafiri mkazi wa Mtaa huo ameiomba serikali kuangalia uwezekano wa kuwasaidia wazee hasa wasio jiweza kwa kuwaingiza katika mfumo wa mfuko wa Maendeleo Jamii Tasaf ili waweze kujikwamua kuichumi.

‘’Ukiangalia huyu Bibi ni Mjane na umri wake umeenda ila siamini kama yupo katika Mfuko wa Tasaf angeunganishwa huko labda angeweza hata kukalabati nyumba yake amesema Msafiri ,,

Mjumbe wa serikali ya Mtaa wa Shanwe lazaro Saimon Kakamba amesema tukio hilo limetokea kwenye mtaa wake na wamesikitishwa na tukio hilo.

Kakamba ameiomba serikali kuangalia uwezekano wazee wasiojiweza kuingizwa katika mfuko wa Tasaf ili waweze kuendesha maisha yao.

‘’Viongozi wanakuja hapa mara tupo kufanya tathimini kila siku tunadangaywa labda 2030 hiyo Tasaf tutaipata’’ amesema Kakamba.

Nyumba hiyo imejegwa zaidi ya miaka 45 iliyopita wakati Khadija Eneliko akiwa na Mme wake.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages