TAYOBECO YASAIDIA JAMII UELEWA NA KUONGEZEKA KWA CHANJO


Meneja   Program wa TAYOBECO  Adinani Mussa akielezea namna mradi wa  Boresha Habari unavyo fanya kazi katika Manispaa ya Mpanda wakati wa kikao cha tathimi toka mradi huu ulipo anza kazi kikao hicho kilicho washirikisha watowa huduma ya afya ngazi ya jamii  na wadau mbalimbali wa afya kimefanyika katika ukumbi wa kichangani Manispaa ya Mpanda

Na Walter Mguluchuma -Katavi

 Idadi ya watu wanaojitokeza kupata chanjo kwenye  vituo mbalimbali vinanyotolea  huduma za  Chanjo imeongezeka kutokana na hamasa kubwa inayotolewa na  na Serikali  na mashirika yasiyo ya kiserikali  ikiwepo taaasisi ya TAYOBECO  na kufanya watu waone umuhimu wa chanjo ya UVIKO 19 na  chanjo za aina nyingine .

Moja ya washiriki wa kikao hicho akitoa maoni yake juu ya mradi huo 
Idadi ya watu wanaojitokeza kupata chanjo kwenye  vituo mbalimbali vinanyotolea  huduma za  Chanjo imeongezeka kutokana na hamasa kubwa inayotolewa na  na Serikali  na mashirika yasiyo ya kiserikali  ikiwepo taaasisi ya TAYOBECO  na kufanya watu waone umuhimu wa chanjo ya UVIKO 19 na  chanjo za aina nyingine .

Hayo yameelezwa na  Mratibu  msaidizi wa Chanjo wa Manispaa ya Mpanda Patrick  Kumburu wakati wa kikao cha taathimini ya utekelezaji wa  mradi wa Boresha Habari  unaotekelezwa katika Manispaa ya Mpanda  na taasisi ya TAYOBECO kilichofanyika katika ukumbi wa Kichangani katika Manispaa ya Mpanda .

Amesema  kuwa idadi ya  watu wanaojitokeza kwenye vituo vya  kutolea chanjo ya Uviko 19 imeongezeka  kufatia wananchi  kupata  uwelewa  kutokana na mradi wa Boresha Habar toka i ulipoanza kufanya kazi kwenye Manispaa ya  Mpanda  kwa kushirikiana na Serikali .

Kumburu  amefafanua kuwa  vyombo vya habari vimesaidia pia  kuwafanya wananchi watambue umuhimu wa  wa huduma ya chanjo ya UVIKO  19  lakini pia hata magonjwa mengine ya mlipuko  wa  janga la surua lililokuwa limeukumba Mkoa wa Katavi .

Hivyo  hata  watowa huduma za  afya  kwa jamii(CHW) hawakuangaika sana kuwafikia wananchi  na kuweza  kupata uwelewa moja kwa moja  juu ya  umuhimu wa hizi huduma za chanjo mbalimbali ambazo zimekuwa zikitolewa kwenye vituo vya kutolea chanjo .

Ametowa mfano wa  chanjo ya UVIKO 19  hapo awali  vituo ambavyo vilikuwa vituo taarifa vilikuwa havifiki kumi  vituo vingine vilikuwa vina sua sua  watu walikuwa na dhana potofu juu ya huduma hizi za chanjo  lakini kutokana na mradi wa TAYOBECO umesaidia sana  kuongeza nguvu ya  uwelewa  kwenye jamii na ndio maana leo wanavituo 28 ambavyo vinalipoti   huduma za UVIKO 19 .

Lakini pia vinaripoti   magonjwa mengine ukiwepo ugonjwa wa mlipuko wa surua  hii  yote imetokana na mchango mkubwa  ambao TAYOBECO  wamewekeza hususani kwa watowa huduma za afyana ndio chanzo cha hayo mafanikio yote  mpaka leo wanafikia idadi kubwa  ya mwitikio wa watu kupata chanjo  na pindi wanapokuwa wameona kuwa na dalili za kupata magonjwa ya mlipuko moja kwa moja wanakwenda kwenye vituo vya kupatia chanjo .

 Program  Meneja  wa   shirika la Tanzania  Youths Behevioral Organization(TAYOBECO)Adinani Mussa amesema kuwa  kwa zaidi ya miaka mitatu  sasa shirika la INTERNEWS Tanzania  limekuwa  likitekeleza  mradi wa boresha habari  unao fadhiliwa na USAID

Lengo la mradi huu     ni kuwahamasisha vijana na  wanawake umuhimu wa chanjo ya Uviko 19  pamoja na chanjo nyingine mbalimbali  ikiwemo chanjo ya surua na  kwa makundi mengine mbalimbali wakiwepo na wazee .

Adinani Mussa amebainisha kuwa kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa hivi karibuni Mkoa wa Katavi ni miongoni mwa mikoa ambayo ilikuwa na mwitikio mdogo wa chanjo ya uviko 19 na ndio maana wakaona mradi huu wa Boresha  habari kuuleta katika  Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi .

Mtoa huduma za afya ngazi ya Jamii katika Kaya ya Mpanda Hotel kwenye kituo cha Afya Mwangaza  Jolald Makori   amesema toka mradi huu  ulipoanza mwanzoni mwa mwezi wa Februali ameweza kuhamasisha watu 441 ambao wameweza kuchanja chanjo ya Uviko 19 ambapo hapo awali kwenye kituo hicho walikuwa hawazidi watu  mia moja .

Ameeleza  kuwa mradi huu watu wameupokea vizuri na watu wamehasika kuchanja   na wala hawakuangaika sana kwa kuwa watu  walikuwa wamehamasika kutoka na elimu iliyotolewa na mradi wa Boresha  Habari .


Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages