SHEKHE MASHAKA: TUIMALISHE UMOJA NA MSHIKAMANO


Shekhe mkuu wa Mkoa wa Katavi Mashaka Nassoro Kakulukulu akitoa neno la shukurani kwenye futari iliyoandaliwa na Eng Isamail Ismail nyumbani kwake eneo la Nsemlwa kwalakwacha
Na Paul Mathias -Katavi.

Jamii katika mkoa wa Katavi imeaswa kuishi kwa upendo na Amani bila kujali itikadi zao ili kuwa na jamii inayomchamungu.

Jamii katika mkoa wa Katavi imeaswa kuishi kwa upendo na Amani bila kujali itikadi zao ili kuwa na jamii inayomchamungu

Wito huo umetolewa na shekhe mkuu wa mkoa wa katavi Mashaka nassoro Kakulukulu wakati akitoa neon la shukurani kwenye Futari Iliyoandaliwa na Eng Ismail Ismail nyumbani kwake Eneo la Kwalakwacha Manispaa ya Mpanda.

Kakulukulu amesema kuwa hiki kinachofanyika cha kujumuika kwa pamoja bila kujali itikakadi wala Imani ya mtu ni ishara upendo na mshikamano kwenye jamii ya wanakatavi.

‘’kitendo hiki kilichofanywa na Ndugu Ismail ni kuonyesha kuwa sisi wanajamii yatupasa kushirikiana katika masuala mbalimbali ya kijamii bila kujali huyu Mwislamu au Mchristo kwa vile Imani zetu zote zinasisitiza umoja Amani na mshikamano’’ amesema Shekhe Mashaka.

Khadija kipingu mkazi wa Kichangani alieshiriki katika Futari hiyo amesema anaishukuru familia ya Eng Ismail kwa kuonyesha upendo kwa jamii kwa kuandaa futari hiyo kwa jamii ikiwa ni sehemu ya kumucha mungu kwa kuonyesha upendo bila kujali Imani ya Mtu.

Nae Emanuel Lupamba mkazi wa Nsemlwa amesema utamaduni kama huu uendelee kwakuwa watanzania tunaishi katika upendo bila kubagua Rangi wala itikadi ya Mtu hivyo tendo hili linaishara ya mshikamano.

‘’Hii inaashiiria umoja na mshikamano tumeweza kushiriki kwenye Futari hii watu wa itikadi tofauti,Amani na umoja ndio msingi wa maendeleo ya wanajamii ‘’amesema Lupamba

Kwa upande wake Eng Ismail Ismail amesema amemua kufanya tendo hilo la kufutulisha ikiwa ni ishara ya upendo inayoambatana na kupata Baraka kutoka kwa mwenyezi mungu kwa kutoa sadaka kama quran inavyo elekeza.

‘’Ninawashukuru wananchi wote waliofika katika hafla hii ya futari niliyoiandaa hapa leo tumejumuika kwa pamoja nimefurahi kuona jamii yangu inajumuika kwa pamoja na mimi kwenye shuguli hii’’amesema Ismail.

Mhandisi Ismail Ismail amesema anaishukuru jamii kwa kumuunga mkono kwa kushiriki katika futari aliyoiandaa.
Awali akitoa salamu za serikali kwa niaba ya Ofisi ya mkuu wa Wilaya ya Mpanda Kenneth Pesambili kaimu Katibu Tawala amesema serikali inatambua mchango mkubwa unaotolewa na viongozi wa Dini katika wilaya ya Mpanda kwa kuilea jamii katika maadili yanayo mcha Mungu.

Futari hiyo imehudhuliwa na Viongozi wa Serikali,Viongozi wa Vyama vya siasa Taasisi na watu Binafsi.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages