Na Paul mathias-Katavi
Baraza kuu la
Waislam (BAKWATA) mkoa wa Katavi limefanya dua maalum ya kumuombea Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kutokana mageuzi makubwa ya
kimaendeleo kwenye utawala wake.
Waumini wa Dini ya kiislamu katika mkoa wa Katavi wakiwa katika Dua Maalumu ya Kumuombea Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan |
Akiwaongoza waumini mbalimbali wa Kiislam mkoani humo, sheikh wa Mkoa wa Katavi Sheikh Mashaka Nasoro Kakulukulu amesema baraza hilo limeamua kumuombea dua hiyo Rais Samia kama shukrani, kwani vitu alivyoufanyia mkoa wa Katavi ni mengi kwa kipindi kifupi na hakuna namna nyingine ya kumlipa.
Aidha amesema hawataishia hapo bali wataendelea kumuombea kila mara ili Mwenyezi Mungu ampe nguvu na utayari wa kuendelea kuwaletea maendeleo watanzania.
Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa
wa Katavi Hassan Rugwa ambaye alikuwa mgeni rasmi katika dua hiyo amewapongeza
waumini wa Kiislam waliojitokeza kushiriki dua hiyo na kuwaomba kuendelea
kumwombea Rais Samia na viongozi wengine kwa Mwenyezi Mungu awaongoze katika
njia bora ya kuwaongoza wananchi.
Nao baadhi ya washiriki wa dua hiyo wamepongeza uongozi wa BAKWATA mkoa wa Katavi kwa kufanya dua hiyo wakidai kuwa kitendo hicho hakijawahi kufanyika na wanaamini kitendo hicho kitampa nguvu na imani zaidi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan na kuendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya kimkakati katika mkoa wa Katavi.
Katika hatua nyingine wadau mbalimbali wameshuliwa kwa kufanikisha shughuli hiyo akiwemo Mbunge wa Jimbo la Mpanda Mjini Sebastian Kapufi kwa kuunga mkono tukio hilo.