WAWILI MBARONI TUHUMA WIZI WA PIKIPIKI

Kamanda wa polisi mkoa wa Katavi,Ali Hamad Makame akizungumnza na waandishi wa habari ofisi kwake kuhusu Matukio mbalimbali katika mkoa wa katavi.

 Na  Walter Mguluchuma .

  Katavi .

Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi  limewakamata watu wawili  kwa tuhuma za  matukio mbalimbali ya kujihusishs  na wizi wa  pipiki  kwenye maeneo mbali  mbali ya wizi wa pikipiki uliokuwa unatokea kwenye Mkoa wa Katavi .

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Ali Makame Hamad amewambia wandishi wa Habari kuwa watuhumiwa hao wamekamatwa kufutia  msako  mkali uliofanywa na jeshi la polisi baada ya kuwa wamepata taarifa ya watu hao kujihusisha na matukio hayo ya wizi .

Kamanda amewataja watuhumiwa hao walio kamatwa na jeshi la  polisi kuwa ni  Benedict Gasper(32)  mkazi wa Mtaa wa Majengo Manispaa ya Mpanda na  Fideris  Ruben  boda  boda Mtaa wa  mtaa wa Airtel Manispaa ya Mpanda .

 Amesema kuwa  katika msako huo watuhumiwa hao wamekamatwa kwa kujihusisha na wizi  wa pikipiki mbili  zenye Namba za usajiri  MC 520 CCK   na pikipiki yenye  Nambza za usajiri   MC128DFU  mali ya   Robbert Ismail .

 Watuhumiwa hao baada ya kuwa wamekamatwa walihojiwa na jeshi la polisi  na baada ya mahojiano na upelelezi kukamilika watuhumiwa hao wote wawili wamefikishwa Mahakamani  na wameisha somewa mashitaka .

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages