KIJANA AFARIKI DUNIA KWA KUCHOMWA NA KISU.

 

waombolezaji wa Msiba katika Mtaa wa Kigoma kata ya Makanyagio Manispaa ya Mpanda Nyumbani kwa mama yake Mzazi Marehemu Kijana Charles Elias alifariki dunia kwa kuchomwa kisu.

Na Paul Mathias- Katavi

Kijana mmoja mkazi wa Mtaa wa Kigoma Kata ya Makanyagio Manispaa ya Mpanda mkoa wa Katavi amefariki dunia baada ya kuchomwa kisu na watu wasiojulikana majira usiku eneo la Mtaa wa kawajense Mpanda Manispaa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi Ali Hamad Makame akizungumnzia tukio hilo ofisini kwake na waandishi wa Habari

Kijana huyo Charles Elias miaka 18 amefariki kwa kuchomwa kisu katika maeneo ya Tumboni na watu wasiotambulika majira ya usiku wa kuamkia 20/4/2023 katika mtaa wa kawajense Manispaa ya Mpanda.

Mama Mzazi wa marehemu Easter Herman amebainisha kuwa asubuhi aliamka na kwenda kazini kwakwe lakini ilipofika majira ya saa nne asubuhi alipata taarifa za mwanawe kufariki Dunia.

Ameeleza kuwa mtoto wake alikuwa anajishughulisha na kazi ya kuuza Barafu na alikuwa amepanga maeneo ya kawajense ambapo alikuwa anafanya shughuli zake huko.

‘’Ilikuwa mda wa saa nne asubuhi nilipigiwa simu na Mdogo wangu nikiwa kazini akaniambia dada una taarifa gani nikamwambia sina taarifa yeyote akaniambia Mtoto wako Charles  amechomwa kisu huko kawajense,, amesema Easter.

Vumilia swila mkazi wa Makanyagio na jirani Nyumbani kwa Marehemu amewaasa wazazi wenzake kuwa na tabia ya kujua mienendo ya kazi za watoto wao wanazo zifanya ili kukabiliana na wimbi la Mmonyoko wa Maadili katika jamii.

Waombolezaji wakiwa katika msiba huo nyumbani kwa mama mzazi wa marehemu Charles Elias Makanyagio Manispaa ya Mpanda.
Swila ameeleza kuwa wazazi wanawajibu wa kuhakikisha watoto wao wanawalea katika misingi ya hofu ya mungu kuanzia wakiwa wadogo.

Kwa upande wake Josephat Katabi mkazi wa Makanyagio amesema kuwa analiomba jeshi la polisi kuimalisha Doria hasa nyakati za usiku ili kukabiliana na uharifu unaoweza kujitokeza.

‘’Niiombe serikali kupitia jeshi la polisi kuimalisha Doria hasa usiku wa manane amabapo matukio haya hutokea ili kuwe na usalama muda wote,, amesema katabi.

Kamanda wa polisi mkoa wa Katavi Ali Hamad Makame amekili kutokea kwa tukio hilo na uchunguzi unaendelea pindi utakapo kamilika jeshi hilo litatoa taarifa kwa wananchi.

Tukio hili la kufariki kwa Kijana Elias Charles linajiri ikiwa ni Takribani wiki moja kwa kijana Michael Chapa mkazi wa Shanwe kuuawa na watu wenye hasila kali kwa kile kilichodaiwa kujihusisha na vikundi vya uharifu maalufu kama damu Chafu.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages