Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Onesmo Buswelu akitoa hotuba ya ufunguzi katika uzinduzi wa Huduma ya M-MAMA kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa katavi. |
Na Walter Mguluchuma
Katavi.
Mkoa wa Katavi
umezindua mpango wa kuwasafirisha kwa
wadharula wajawazito waliojifungua na watoto wadogo kutoka
kituo kimoja kwenda kwenye kituo kingine baada ya kupata uzazi nje
ya kituo cha kutolea huduma ili kuweza kupunguza vifo vya mama na mtoto
kwa kushitikisha jamii.
Wadau mbalimbali wa sekta ya afya katika mkoa wa Katavi wakiwa katika uzinduzi wa huduma ya M-MAMA |
Mkoa wa Katavi umezindua mpango wa kuwasafirisha kwa wadharula wajawazito waliojifungua na watoto wadogo kutoka kituo kimoja kwenda kwenye kituo kingine baada ya kupata uzazi nje ya kituo cha kutolea huduma ili kuweza kupunguza vifo vya mama na mtoto kwa kushitikisha jamii.
Uzinduzi huo wa Mradi
umezinduliwa na Mkuu wa Mkoa wa Katavi ambae aliwakilishwa kwa niaba yake
na Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Onesmo Buswelu uzinduzi ambao uliudhuriwa na
viongozi mbalimbali kutoka Halmashauri zote za Mkoa wa Katavi pamoja na
wataalamu kutoka Wizara ya Afya .
Mganga Mkuu wa Mkoa wa
Katavi DKT jonathan Budenu amesema kuwa lengo la mradi
huu ni kushirikisha jamii kusafirisha wajawazito
wanaojifungua na watoto wachanga ili kuwasafirisha kutoka kituo kimoja
kwenda kwenye kituo kingine pindi wanapokuwa wamejifungua nje ya kituo ili
kuokoa vifo vya mama na mtoto vinavyosababishwa na watu kukosa
usafiri wa kuwafikisha kwenye vituo vya kutolea huduma za afya .
Amebainisha
kuwa wanajua kwamba moja ya masuala wanayohitaji
kuyafanyia kazi ni rufaa kati ya vituo vya kutolea huduma za
afya ,afya hasa upatikanaji wa usafiri wa dharula
kutoka kituo kimoja hadi kituokingine kinachoweza kutoa
huduma kwa kiwango cha juu na pia ukosefu wa usafiri wa
dharula kutoka kwenye jamii hadi kwenye vituo vya kutolea huduma .
Mradi huu wa M-
MAMA utasaidia sana kwani kwa sasa Mkoa wa Katavi unajumla ya
magari sita tuu ya kubebea wagonjwa kwa Mkoa mzima yanayofanya kazi
ya kutowa huduma za dharula kwa wagonjwa kwenye vituo vya
kutolea huduma za afya .
Msitahiki meya wa Manispaa ya Mpanda Haidary Sumry akitoa katika uzinduzi huo kwa kuwa hakikishia wananchi wa manispaa ya Mpanda kuwa mpango huo utatekelezwa kwa malengo yaliyo kusudiwa |
Katika hotuba ya
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoka kwenye uzinduzi wa mradi huu
uliyosomwa kwa niaba yake na mwakilishi wake ambae ni Mkuu wa Wilaya ya
Tanganyika Onesmo Buswelu amesema Mkoa sasa unauhakika
changamoto hiyo iliyokuwepo itatatuliwa na mfumo huu wa
usafirishaji wa dharula .
Ambao Serikali
imefanya kazi na wadau mbambali wa maendeleo VODA COM/VODA
FONE na washirika wake ambao ni Touch Found ation
na Pathfinder International katika uzinduzi
huu wameweza kupata maelekezo juu ya ufanyaji kazi wa
mfumo huu ili viongozi wa ngazi mbalimbali wawe sehemu ya
utekelezaji wa mpango kwa kutambua wajibu na
majukumu yao katika kutekeleza mpango husika .
Amesema mfumo huu huu wa M- MAMA utahakikisha kuwa vituo vya kutolea huduma za afya ngazi ya chini zanahati na vituo vya Afya na wale wenye dharula walipo kwenye jamii wanapata usafiri wa dharula utaopatikana muda wote .
Kwa kuwa magari ya kubeba wagonjwa yapo machache kwa mfumo huu watachagua magari machache ya watu binafsi watakayoyachagua na kuwatambua wamiliki wa magari katika kila Kata na kuingia nao mikataba kupitia Halmashauri na madreva wa magari yatakayokuwa yamechaguliwa wataingizwa kwenye mfumo wa M- MAMA ambao unaendeshwa na serikali kwa kushirikiana na wadau wengine .Wadau watahusika
kutowa huduma za usafiri wa dharula pale tuu magari ya
serikali ya ubeba wagonjwa yanapokuwa yamekosekana kwa sababu
mbalimbali zinazo eleweka muhimu ni kuhakikisha
kila mama mwenye dharula anafikishwa sehemu
stahiki ili aweze kupata huduma bora kwa wakati .
Meya wa Manispaa ya Mpanda Haidari Sumry amesema kuwa Manispaa ya Mpanda itahakikisha inatowa ushirikiano wa kutosha kwenye mlagi huu kwa kuwa ni mradi muhimu na unalenga kuokoa vifo vya akina mama na watoto