Waumini wa umoja wa Makanisa ya Kipentekosti Wilaya ya Nkasi Mkoa wa Rukwa wakiwa katika maandamano ya amani ya kupinga vitendo Ushoga.
Na Israel Mwaisaka,Rukwa
umoja wa makanisa ya Kipentekosti Tanzania
wilayaNkasi mkoani Rukwa (CPCT) wamefanya maandamano ya amani kupinga
vitendo vya ushoga huku wakiishinikiza serikali kuendelea kuchukua hatua kali
dhidi ya watakaobainika kujihusisha na vitendo hivyo haramu.
Umoja wa makanisa ya Kipentekosti Tanzania wilayaNkasi mkoani Rukwa (CPCT) wamefanya maandamano ya amani kupinga vitendo vya ushoga huku wakiishinikiza serikali kuendelea kuchukua hatua kali dhidi ya watakaobainika kujihusisha na vitendo hivyo haramu
Mwenyekiti wa CPCT wilayani Nkasi Mchungaji Efraimu Lyanduru amesema kuwa wao kama viongozi wa dini wanapinga vikali vitendo hivyo vya ushoga na usagaji kwani ni mambo yanayokwenda kinyume na matakwa ya Mungu na kuwa wanaungana na serikali katika mapambano hayo.
Amesema kuwa vitendo vya ushoga kuendelea kushamiri duniani ni ishara tosha ya ukengeufu wa maadili miongoni mwa jamii na kuwa vitendo hivyo ni kinyume kabisa na tamaduni zetu za Kiafrika na kudai kuwa vita hii sasa ni ya kila mmoja.
Mchungaji Lyanduru amedai kuwa licha ya serikali kuonyesha nia ya kukabiliana na vitendo hivyo bado wanaiomba iongeze mapambano kwa kutowaonea aibu watu wale wote wanaojishughulisha na vitendo hivyo dharimu ikiwa ni kuendelea kutunga sheria kali dhidi ya watu hao.
Katibu wa CPCT Mchungaji Fidelis Maheke amesema kuwa vitabu vitakatifu vyote kwa maana ya Biblia na Quran vyote vinapinga vitendo hivyo na kuwa vinaeleza kuwa yanapotokea mambo hayo ni viashiria vibaya na kuwa ndiyo wakati wa viongozi wa dini kuchukua hatua kwa kuitahadharisha jamii kuchukua hatua kwa kuingia kwenye mapambano hasa maombi.
Amesema kuwa ukisoma kitabu cha Walawi 20:3 inakemea vitendo vya ushoga na kuwa huo ni mpango wa shetani ili uzao usiendelee kwa maana vitendo hivyo vya ndoa ya jinsia moja havina mwendelezo wa uzazi kwa jamii na kuwa hizo ni ishara za mwisho wa dunia hivyo ni muhimu kwa kila mmoja kuchukua hatua hasa kuingia katika maombi kuliombea taifa na dunia kwa ujumla.
Baadhi ya Wazazi na walezi wilayani humo wamesema kuwa ni wakati sasa kwa serikali kulichukulia uzito wa aina yake jambo hilo ikiwa hata kutunga sheria kali dhidi ya wanaojihusisha na vitendo hivyo vya ovyo.
Greener Sanga alidai kuwa wao kama wazazi vitendo hivyo vinawafanya kukosa amani hasa ukichukulia kuwa vitendo hivyo vinafanywa na Watoto wao na kuomba kila mmoja kulipigia kelele jambo hilo kwani ni baya sana katika jamii.
Amesema kuwa umefika wakati kwa kila mzazi kufuatilia nyendo za Watoto wao na kuchukua hatua za haraka pale wanapobaini vitendo hivyo kuwepo lakini kubwa ni kutoa taarifa serikalini ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa.
Lejas Mlumbe kwa upande wake alidai kuwa ushoga na usagaji ni hila la shetani katika kuharibu jamii hivyo ni muhimu kila mmoja kuingia katika vita hiyo tusiiachie serikali na viongozi wa dini pekee bali kila mmoja akiingia kwenye mapambano haya tunaamini kabisa vitendo hivyo vitatoweka.
Maandano hayo ya kupinga vitendo vya ushoga na usagaji vilienda sambamba na kuliombea taifa na kumlilia Mungu ili aweze kuuokoa ulimwengu dhidi ya vitendo hivyo