Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko akizungumnza na wanachi juu ya umuhimu wa kutunza mazingira na upandaji miti |
Na Walter Mguluchuma
Katavi
Mkoa wa Katavi
wametekeleza agizo lililotolewa na Makamu wa Rais Dkt Philpo
l Mpango la kuzitaka kila Halmashauri za hapa nchini kupanda miche
ya miti kwa kila Halmashauri zisizopungua milioni moja na nusu .
Mkuu wa mkoa wa Katavi, Mwanamvua Mrindoko akipanda mti katika shule ya Sekondari Anna Lupembe
Mkoa wa Katavi wametekeleza agizo lililotolewa na Makamu wa Rais Dkt Philpo l Mpango la kuzitaka kila Halmashauri za hapa nchini kupanda miche ya miti kwa kila Halmashauri zisizopungua milioni moja na nusu .
Mkuu wa Katavi
Mwanamvua Mrindoko amewambia wananchi wa Halmashauri ya
Nsimbo leo wakati wa zoezi la upandaji miti uliofanyika katika shule ya
Msingi Isinde kuwa hadi sasa Mkoa wa Katavi kupitia kwa Halmashauri zake tano
za Mkoa huu zimeisha panda zaisi ya miche za miti zaidi ya milioni 6 na laki
tisa.
Amebainisha kuwa Mkoa huu
bado unaendelea na zoezi hilo la upandaji miti ambapo idadi hiyo ya miti
iliyopandwa ni kwenye awamu yao ya kwanza kwenye zoezi hilo na sasa
wanaingia kwenye awamu ya pili ya upandaji miti hali ambayo inaonyesha kuwa watapanda
miti mingi kuliko idadi waliopangiwa .
Kwani Mkoa wa
Katavi umejiwekea uutaratibu wa kupanda miti na kutunza mazingira kuwa ni
utaratibu endelevu ili mkoa huu uendelea kuwa wa kijani zaidi kuliko ulivyosasa
licha ya kuwa wakijani .
Ameeleza kuwa zoezi la
upandaji miti ulifanywa mwishoni mwa mwezi wa pili mwaka huu kwa awamu ya
kwanza na awamu ya pili itafanyika mwanzoni mwa mwezi mei kutokana
na msimu wa mvua za masika haribu unakwisha .
Maelekezo ya
Makamu wa Rais na Rais kupitia Wizara ya Mazingira yanaelekeza kila
Halmashauri kufikia lengo kama walivyopangiwa kwa hiyo kwa Mkoa wa Katavi hadi
sasa wamebakiza miti michache sana ili kufikia lengo walikupangiwa
hivyo wataendelea kupanda miti zaidi ya milioni saba walipangiwa kwa
msimu huu.
Amesisitiza kuwa zoezi
hili la upandaji miti sio la shoo kwani lazima miti yote iliyopandwa itunzwe na
ikuwe na ilindwe isiharibiwe na binadamu wala wanyama waharibifu
lazima ikuwe na iweze kuleta manufaa yaliyokusudiwa
Mrindoko amezita taasisi
za umma kuhakikisha zinapanda miti na watapita kuzikagua kila
wanapokuwa wanapita kukagua miradi ya maendeleo watakuwa wanakagua na miti
iliyopandwa kwani kamati yake ya kukagua ipo imara sana
Aidha Rc Mrindoko
alisema kuwa maadhimisho ya Muungano wa Tanzania Zanzibar na Tanzania
Bara yalianza Aprili 17 na yameitimishwa leo Aprili 29 Nchi
nzima kwa maelekezo yaliyotolewa na Serikali kwamba maadhimisho
yafanyike kwa ngazi ya Mkoa na Wilaya zake na yaendelee mpaka tarehe 29
kwa hiyo tarehe ya muungano ina baki ile ile .
Amewataka wananchi
wa Mkoa wa Katavi kuendelea kuulinda na kuutunza Muungano ili uwendelee
kudumu kwani miaka 59 sio michache ni jambo la kujipongeza kwani nchi
yetu imeweza kuuwendeleza Muungano na mpaka sasa hivi hatuja farakana
kati ya Tanzania Bara Tanzania Visiwani .
Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Nsimbo Mohamed Ramadhani ameeleza kuwa Halmashauri hiyo mbali ya
kupanda miti kwenye maeneo mbalimbali wameendelea pia na upandaji
miti kwenye maeneo ya pembeni ya barabara za Halmashauri ya Nsimbo .
Lengo la Halmashauri hiyo
pia ni kuhakikisha kila mwananchi anapokuwa anapita barabarani atakuwa anapita
kwenye kimvuli ya miti itakayokuwa pembeni mwa barabara .
Mbunge wa Jimbo la Nsimbo
ambae pia ni Makamu mwenyekiti wa Kamati ya Maji na Mazingira Anna Lupembe
amesema kuwa Benki ya NMB wameisha towa ahadi ya kutowa kiasi cha shilingi
milioni 50 kwa Halmashauri ambayo itafanya vizuri kwenye zoezi la upandaji wa
miti .
Hivyo ataendelea
kuwahamasisha wananchi wa Nsimbo kuendelea kupanda miti ili waweze kupata
fedha hizo watakazo zitumia kujenga madarasa kwenye shule moja ya msingi .