Mkuu wa mkoa wa Kaavi Mwanamvua Mrindoko akipata maelezo kuhusu Mpira wa Pete kwenye bonanza lililoandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Nsimbo Anna Lupembe. |
Na Walter Mguluchuma.
Katavi .
Timu tano za mpira wa Kikapu
kutoka mikoa mitano ya Dodoma , Rukwa ,
Kigoma,Tabora na Katavi zimeshiriki
bonanza la mchezo wa mpira wa kikapu kwenye uzinduzi wa viwanja vya michezo ya
mpira wa kikapu na mpira wa pete Bonanza
ambalo liliandaliwa na Mbunge wa Jimbo
la Nsimbo Anna Lupembe .
Timu tano za mpira wa Kikapu kutoka mikoa mitano ya Dodoma , Rukwa , Kigoma,Tabora na Katavi zimeshiriki bonanza la mchezo wa mpira wa kikapu kwenye uzinduzi wa viwanja vya michezo ya mpira wa kikapu na mpira wa pete Bonanza ambalo liliandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Nsimbo Anna Lupembe . Moja ya Muonekano wa Kiwanja cha Mpira wa Kikapu kilicho zinduliwa kwenye Bonanza hilo
Bonanza hilo lililohudhuriwa na mamia ya wanamichezo na wananchi
wa Mkoa wa Katavi ambapo mgeni rasmi
alikuwa Mkuu wa wa Katavi
Mwanmvua Mrindoko pia bonanza hili lime hudhuriwa na Rais wa shirikisho la mpira wa kikapu Tanzamia
Michael Kadebe
Akinzumza kabla ya
uzinduzi wa viwanja hivyo viwili
vilivyojengwa katika shule
ya Sekondari Nsimbo Mbunge wa
Jimbo hilo Anna Lupembe ameeleza kuwa viwanja hivyo viwili vya mpira wa pete na vikapu amevijenga kwa gharama ya zaidi ya
shilling Milioni 50 zilizotokana na fedha za mfuko wa jimbo .
Aliamua kuwekeza kwenye sekta ya michezo kwa kujenga viwanja
hivyo viwili na kimoja cha mpira wa miguu kwa kutambua kuwa michezo ni afya na
ajira kwa vijana kwa sasa michezo ni ajira nzuri kwa vijana na ndio maana ameamua kujenga viwanja vya
aina mbalimbali kwa ajiri ya kuinua vipaji na afya pia kwa watu wazima kwa kuwa
watu wengi wanaandamwa na magonjwa mengi .
Lupembe amesema kwa wao
kama viongozi wanaiga wanaiga
mfano wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutowa hamasa kwenye sekta ya
michezo hapa nchini ili vijana
wapate ajira kwa kupitia michezo .
Amebainisha kuwa kwa
kutambua umuhimu wa michezo ameanzisha mashindano ya
mpira wa miguu yanayoitwa Lupembe
Cup na kwa mwaka jana timu 140 zilishiriki mashindano hayo ameona ameona bi vema kuibua vipaji vya
michezo mingine mbali ya mpira wa miguu na
ndio maana ameamua kufanya bonanza la mpira wa vikapu na pete ili kuinua vipaji
kwa vijana .
Rais wa shirikisho wa shirikisho la mpira wa vikapu Tanzania Michael Kadebe amesema kuwa kupitia kwa bonanza hilo kutasaidia sana kuleta chachu na hamasa kwa wanamichezo kupenda kuchezo michezo ya mpira wa vikapu na pete kwani bado kuna furusa kwa vijana .
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko amewaagiza wakurugenzi
wote wa Halmashauri kuhakikisha miundo mbinu ya michezo inaboreshwa na michezo
inachezwa mashuleni kuanzia shule za msingi .