Na Paul Mathias
Katavi.
Chama cha Mapinduzi CCM Katika Mkoa wa Katavi kupitia Kwa Mjumbe
wa Halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM Taifa Girbert Samnpa katika Mkoa
wa Katavi ametoa Wito kwa Jumuiya ya wa wazazi ya Chama hicho kuungana na
serikali katika kukemea Mmomonyoko wa Maadili katika Jamii.
Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Katavi kupitia Kwa Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM Taifa kutoka Mkoa wa Katavi Girbert Samnpa ametoa Wito kwa Jumuiya ya wa wazazi ya Chama hicho Mkoa wa Katavi kuungana na serikali katika kukemea Mmomonyoko wa Maadili katika Jamii.
Ametoa wito huo wakati akifungua maazimisho ya Wiki ya Jumuiya ya Umoja wa wawazi ya Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Katavi yaliyofanyika katika Shule ya Msingi Itenka Halmashauri ya Nsimbo Mkoa wa Katavi.
Baadhi ya wanachi na wanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM kata ya Itenka walivyojitokeza katika uzinduzi wa Wiki ya Jumuiya ya wazazi iliyofanyika kimkoa katika kata Hiyo. |
‘’Anasema kwa hali ya sasa hii Jumuiya kama chama cha Mapinduzi
kinaitazama sana Jumuiya ya wazazi mmomonyoko wa maadili ambao umekuwa Janga
kwa sasa kitaifa na Kidunia’’
Ameeleza kuwa Chama cha Mapinduzi CCM kinaitizama Jumuiya hiyo kama Kitengo Maalumu kwa kuwandaa viongozi wanaochipukia kwenye Ungozi ndani ya chama na Jumuiya kuwa katika maadili na kukemea vitendo vya Mmomonyoko wa maadili katika Jamii.
Katika hatua nyingine amesema Jumuiya ya wazazi imekuwa mlezi
kwakuwa imekuwa ijajihusisha Moja kwa moja katika Malezi na Elimu kwa Vitendo
zaidi ndani ya chama.
‘’sisi kama chama cha Mapinduzi ndio walezi wetu kupitia jumuiya
hii inadili na malezi jumuiya imejikita kwenye Elimu kwa vitendo ndio Jumuiya yenye
shule nchi nzima zilizopo chini ya Jumuiya ya wazazi’’amesema Samnpa.
Ameeleza kwa sasa chama hicho kimekuja na sera ya kuimalisha
uchumi kuanzia ngazi ya jumuiya za chama ili kukisaidia chama katika mambo
mbalimbali yanayo hitaji uchumi kiuendeshaji katika Shughuli mbalimbali.
amewaomba wananchi na wanachama wa chama hicho kuendelea kukiamini chama cha Mapinduzi kwakuwa kinatekeleza ilani kwa Vitendo kwenye Miradi ya Maji,Afya,Elimu na miundombinu Chini ya Mwenyekiti wa Chama hicho Rais Dk Samia Suluhu Hassan
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya Wazazi Mkoa wa Katavi Evarist
Mnyere amesema Moja ya Majukumu ya Jumuiya hiyo ni Kusimamia Mazingira Malezi
na Elimu na ndio maana zoezi la upandaji miti limefanyika katika Kiwanja cha
CCM Kata ya Itenka na Kituo cha afya Itenka.
Mnyere ‘’anasema Jumuiya hii inasimamamia Mazingira,Elimu na
Malezi hivyo jumuiya hii ni Jumuiya mama katika chama chetu,,
Uzinduzi huo wa Wiki ya Jumuiya ya wazazi ya Chama Cha Mapinduzi
CCM katika mkoa wa Katavi imeenda sambamba na Upandaji wa miti katika Kiwanja
Kinachomilikiwa na Chama cha Mapinduzi CCM Kata ya Itenka,Kufanya Matendo ya
Huruma kwa kuwajulia hali wagojwa katika Kituo cha Afya Itenka pamoja na
kupanda miti kwenye Kituo hicho.Mjumbe wa Halmashauri kuu ya chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Katavi Girbert Samnpa akipanda mti katika kiwanja kinachomilikiwa na chama cha Mpainduzi CCM Kata ya Itenka.
Sherehe hizo za Maadhimisho ya Wiki ya Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi CCM itahitimishwa kitaifa katika mkoa wa Manyara.