Na Paul Mathias
Katavi,
Vijana katika Mkoa wa Katavi
wameaswa kuchangamkia fursa ya utoaji wa huduma za kifedha za Kibenki kwanjia ya uwakala
Kupitia Benki ya CRDB benki ikiwa ni sehemu ya kukabiliana na tatizo la ajira kwa
vijana hapa nchini.
Wito huo umetolewa na Msitahiki
meya wa Manispaa ya Mpanda Haidary Sumry wakati akifungua semina maalumu kwa watoa
huduma za kifedha katika mkoa wa Katavi wanaotoa huduma za kifedha kwanjia ya
uwakala ikiwa ni sehemu ya kufikisha miaka 10 kwa huduma hiyo kuazishwa katika
Benki ya CRDB kote nchini.
Haidary amesema kuwa Vijana wa
Mkoa wa katavi hawana budi kuchangamkia fursa ya kuwa sehemu ya kutoa huduma za
kifedha kwa kuwa Mawakala ikiwa ni sehemu inayotolewa na Benki ya CRDB Benki
kama sehemu ya kukabiliana na changamoto ya ajira kwa vijana.
‘’nimeambiwa hapa kwa Nchi nchi nzima CRDB benki mnamawakala zaidi ya elfu 25000 nchi nzima na hapa katavi kuna mawakala zaidi ya 60 kwahiyo kati ya hao elfu 25000 na vijana wa katavi wamo hii ni fursa kubwa ambayo mmepewa na Benki ya CRDB benki itumieni vizuri kwa kukuza uchumi wa taifa na uchumi wenu kwa ujumla’’
Amesema huduma hizo za kifedha kupitia Mawakala wa kifedha wa CRDB Benki imelahisisha katika malipo mbalimbali ya kiserikali pamoja na ada za shule kwa wazazi na walezi kupitia huduma zinazo tolewa na Benki ya CRDB benki kwa mawakala wao kwenye maeneo mbalimbali ya mkoa wa katavi.
Haidary amesema kuwa CRDB benki
kwa nchi nzima imeweza kutoa ajira zaidi ya Elf 35000 nchinzima hatua hiyo ni
sehemu ya kukabiliana na tatizo la ajira kwa vijana hapa nchini.
Amefafanua kuwa Katika kukuza
uchumi wa taifa ‘’Benki ya CRDB benki kwa mwaka hufanya miala milioni Miamoja
yenye thamani ya Shilingi Trion 50
ambapo kati ya hizo Trioni 1.3 nimapato ya serikali kwa kazi hii
mnayoifanya mawakala mnaisadia sana serikali katika ukusanyaji wa mapato’’
Meneja wa Benki ya CRDB Mpanda Hamad Masoud [Kushoto] akimkabidhi cheti moja ya washiriki wa semina ya kuadhimisha miaka 10 tangu huduma ya CRDB wakala ilipoanza kufanya kazi hapa nchini. |
Hamad Masoud Meneja wa Benki ya CRDB Benki tawi la Mpanda amesema kuwa tangu huduma hiyo ya utoaji wa huduma za kifedha kwa mawakala umekuwa na msaada mkubwa kwa wananchi kwa kuepusha Gharama na usumbufu ambao ulikuwa unapatikana katika malipo mbalmbali ya fedha kiserikali na mtu mmoja mmoja.
‘’tunajivunia huduma hii ya CRDB wakala kwa kipindi cha miaka 10 tumekuwa karibu zaidi na wateja wetu kupitia Mawakala hawa ndio maana tunasema CRDB benki ulipotupo’’ amesema Hamad
Mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Katavi Resort Mjini Mpanda kwa kuwa husisha zaidi ya mawakala 60 wa huduma za kibenki kutoka Benki ya CRDB Benki kutoka sehemu mbalimblali katika mkoa wa katavi.