Na Paul Mathias
Katavi,
Mkuu wa mkoa wa Katavi mwanamvua Mrindoko ameziagiza taasisi za serikali kujiwekea mikakati ya kupanda miti Milioni moja kwa kila taasisi ikiwa nisehemu ya mwendelezo wa upandaji miti katika kukabiliana na Mabadiliko ya Tabia nchi.
Mkuu wa mkoa wa Katavi mwanamvua Mrindoko ameziagiza taasisi za serikali kujiwekea mikakati ya kupanda miti Milioni moja kwa kila taasisi ikiwa nisehemu ya mwendelezo wa upandaji miti katika kukabikaina na Mabadiliko ya Tabia nchi.
Ameyasema
hayo wakati akikabidhiwa miti 1000 na Shirika lilisilokuwa la kiserikali
Nilinde Community Organization kwaajili ya kupadwa katika taasisi Mbambali
mbali za umma.
Mrindoko
amesema ‘’nitoemaelekezo kwa taasisi za serikali kuhakikiasha mnajiwekea lengo
la kupanda miti million Moja kwa kila taasisi kama sehemu ya mwendelezo wa
zoezi la upandaji miti kwenye taasisi zenu kama wewe ni mkuu wa taasisi na upo
hapa kafanye hivyo ili uendelee kuitwa mkuu wa taasisi hiyo ‘’
Amesema
kuwa kwakuwa suala la upandaji miti nia agenda ya kitaifa hivyo kila mwanachi
katika mkoa wa Katavi anaowajibu wa kushiriki katika zoezi la upandaji miti kwa
lengo kuhifadhi mazingira.
Ameeleza kuwa miti hiyo iliyotolewa na taasisi ya Nilinde Community Organization ikapadwe katika shule za msingi na sekondari kulingana na mahitaji ya shule husika katika maeneo yao ili kuunga mkono juhudi za serikali katika suala la utunzaji wa Mazingira.
‘’niombe
walimu mliopo hapa hakikisheni Miti hii tuliyopatiwa leo mnakwenda kuisimamia
ipandwe vizuri kwenye maeneo yenu ya shule na muisimamie ukue na isitwi’’
Katika
hatua nyingine mkuu huyo wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko ameipongeza
taasisi ya Nilinde Community Organization kwa kuona umuhimu wa kushiriki katika
utunzaji wa mazingira kwa kuotesha miche ya miti na kuigawa kwa serikali.
Awali
akitoa taarifa kwa mkuu wa mkoa Mkurugenzi wa Shirika la Nilinde Organization
Alinanuswe Edward amesema kuwa Shirika hilo limekuwa likitoa Miti ya Matunda kwa taasisi mbalmbali zikiwemo shule za msingi
na sekondari katika mkoa wa Katavi.
Alinanuswe
‘’anasema Mwaka 2022 mwanzoni shirika lilitoa miti ya Matunda 1200 kwa shule za
msingi na sekondari mkoani hapa kwaajili ya kuunga mkono juhudi za mkoa katika
kukabiliana na lishe duni hali inayopelekea udumavu’’
‘’katika
kuunga mkono juhudi za mkuu wa mkoa wa Katavi kuifanya Katavi iwe ya kijani mwaka
jana shirika lilitoa Miti 450 na kukabidhi kwa Afisa mazingira wa Manispaa ya
Mpanda’’ amesema Alinanuswe
Amesema lengo la shirika nikuhahakisha mazingira yanatuzwa kwa kizazi cha sasa na kijacho ndio maana wameamua kakabidhi miti 1000 kati ya 6000 mbayo wameamua kuitoa kwa serikali katika mkoa wa Katavi.