Na Paul Mathias
Katavi,
Wananchi katika mkoa wa Katavi
wameaswa kuendelea kulinda Tunu za muungano wa Tanganyika na Zanzibari ulio
asisiwa na Viongozi wazalendo wa Taifa la Tanganyika na zanzibari Hayati Abeid
Aman Karume na Julias Kambarage Nyerere Mnamo 26/4/1964.
viongozi mbalimbali wa Halmashauri na wilaya wakiwa katika maadhimisho ya miaka 59 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar yaliyofanyika kimkoa katika Halmashauri ya Mpimbwe eneo la Usevya. |
Akiwa hutubia wanachi wa mkoa wa Katavi katika maadhimisho ya kumbukizi ya miaka 59 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar yaliyofanyika kimkoa katika halmashauri ya Mpibwe Eneo la viwanja vya Sharp Rangers Usevya.
Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko
amesema muungano huo ishala ya umoja na mshikamano kwa wanachi wa Tanzania Bara
na Tanzania Visiwani.
Mrindoko ameeleza kuwa muungano
umeweza kukuza uchumi kwa wanachi kwakuwa wananchi kutoka Tanzania Bara na
wananchi kutoka visiwani Zanziba wanao uhuru wa kufanya shughuli za kiuchumi
pasipo na kikwazo chochote hali ambayo huimalisha uchumi kwa wananchi kupitia
shughuli za kiuchumi.
Katika hatua nyingine Mrindoko
ameeleza kuwa kuna faida kubwa ya muungano hasa katika eneo la ulinzi na
usalama wa mipaka ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania hali hii husaidia katika
kuendeleza Amani na utulivu katika kulinda Rasilimali za nchi kwa manufaa ya
wananchi na maendeleo kwa wananchi.
Amesema katika kuendelea kuenzi Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni muda muafaka sasa kwa wazazi na walezi kuendelea kuwaelimisha watoto juu ya umuhimu wa muungano wa Tanganyika na Zanzibari ili kuwa na kizazi kitakachokuwa na uelewa kuhusu muungano huu adhimu kwenyye Jamuhuri ya muungano wa Tanzani.
Ikumbukwe kuwa Muungano huu wa
Tanganyika na Zanzibar umebaki kuwa muungano imala hali ambayo inatimiza ndoto
za viongozi waasisi wa Mataifa ya Afrika
akiwemo hayati Mwalimu Julius Kambarage
Nyerere pamoja na baadhi ya viongozi waasisi wa Mataifa ya Afrika kama Kwame Nkrumah
wa Ghana pamoja na viongozi wengi wa afrika amabao walitamani afrika iungune
ndoto ambazo hazikufanikiwa kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo mifumo
tofauti ya kiutwala iliyokuwa chini ya ukoloni kwenye Mataifa yao.
Maadhimisho hayo yameenda sambamba na kauli mbiu inayosema MIAKA 59 YA MUUNGANO NDIYO NGUZO YA KUKUZA UCHUMI WETU, Kwa sisi wazalendo wa Taifa hili sote tuseme udumu Muungano wa Tangayika na Zanzibar.