Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Katavi ACP Ali Makame Hamad akitoa taarifa mbalimbali za utendaji kazi wa Jeshi hilo Mbele ya waandishi wa Habari ofisi kwake. |
Na Paul Mathias.-Katavi
Jeshi la polisi mkoa wa limewakamata watoto 15 wanaojihusisha na makundi ya uharifu katika umri Mdogo ambayo yamekuwa yakijukiana kwa majina ya Damu chafu na Manyigu.
Vitu mbambali vilivyokamatwa na polisi vinavyosadikiwa kuwa nivyawizi
Jeshi la polisi mkoa wa limewakamata watoto 15 wanaojihusisha na makundi ya uharifu katika umri Mdogo ambayo yamekuwa yakijukiana kwa majina ya Damu chafu na Manyigu.
Akitoa taarifa mbele ya waandishi ya utendaji kazi ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi Kamanda wa Polisi mkoa wa Katavi Ali Hamad Makame amesema jeshi hilo kupitia misako mbalimbali limeweza kuwa kamata watoto hao pamoja na wazazi wao na kufikishwa mahakamani na kulipa faini ya Shilingi 50000/=.
Kamanda
Makame amewaonya vikali wazazi na walezi
amabao wamekuwa wakiwatumikisha watoto wao kwa kufanya shuguli za kiuchumi kwa
kuuza baiashara ndogo ndogo mitaani badala ya kuwapeleka watoto hao shule na
kusisaitiza kuwa jeshi hilo halitakuwa na simile kwa mzazi au mlezi wa mtoto
ambae atabainika kumtumikisha mtoto wake katika biashara ndogo ndogo mtaani.
Ameeleza
kuwa Mpaka sasa kuna msako mkali unaendelea kufanyika katika maeneo mbalimbali
ya mkoa wa Katavi ya kuhakikisha watoto wadogo hawajihusishi na Biashara muda
wa Masomo huku baadhi yao kujiingiza
katika vikundi vya kiharifu.
‘’Tunaendelea
kufanya Msako wa kuwakamata watoto wadogo wanaofanya baiashara ndogo ndogo na
katika hili hatutakamata mtoto pekee tutamkamata hadi Mzazi wake ili atuambie
kwanini mtoto anampa majukumu ya kutunza familia wakati mzazi na mlezi upo’’
Vitu mbambali vilivyokamatwa na jeshi la polisi ambavyo vinasadikiwa ni mali za wizi |
Katika hatua nyingine makame amewaomba wazazi kuzingatia malezi ya watoto kwakuzingatia maadili ya utanzania na kuwalea watoto katika misingi ya hofu ya mungu ili kutengeneza kizazi ambacho hakina tabia za uharifu katika siku za usoni.
‘’tusemetu
kwamba suala hili la malezi ya Watoto
linaumuhimu wa kipekee kwa watoto waliochini ya umri wa miaka 18 hawa wanatajwa
kwamba wanakianzana na sheria maana yake bado wazazi wanalojukumu la
kuhakikisha kwamba wanawasimamaia vyema watoto wao kwani umri huo niwawatoto
kwenda shule lakini wanaachiwa mitaani na hatimae kuingia katika wimbi la
uharifu sisi kama jeshi tutaendelea kutekeleza wajibu wetu na sisi kama jeshi
la Polisi tutakamata mtoto na mzazi wake
ambae atakwenda kinyume kwa kuwatumikisha watoto au mtoto wa mazazi fulani kujiingiza
katika makundi ya uharifu’’
Jamii
kwa ujumla lazima iwe sehemu ya kuhakikisha watoto wanalelewa katika misingi ya
malezi bora na maadili kuanzia ngazi ya familia ili kuepuka wimbi la mmomonyoko
wa Maadili kwa watoto na kukua katika mwenendo mwema ili kuwa na jamii yenye
Tabia njema.
Katika
taarifa hiyo jeshi lapolisi mkoa wa katavi limeweza kuwakamata watuhumiwa 214
wa makosa ya mali za wizi na watuhumiwa 14 wakijihusisha na uharifu wa wa makossa
ya uvunjaji na kuiba vitu mbalimbali kama Redio,Jogofu,Tv tatu,Mageti ya chuma
ya milango 40.
Wananchi wameobwa kufika kituo cha Polisi Mpanda kwaajili ya utambuzi wa vitu vyao wakiwa na vielelezo vya uhalali wa ununuzi wa vifaa hivyo kabla ya kuibiwa.