Vifaa Tiba vilivyo tolewa na serikali katika Hospitali ya Wilaya ya Nkasi Mkoa wa Rukwa nye Thamani ya Shilingi Bilion 1.8 |
Na
Israel Mwaisaka,Nkasi
Wilaya
ya Nkasi imepokea vifaa tiba na dawa vyenye thamani ya shilingi Bilioni 1.8 kwa ajili ya Hospitalii ya Wilaya, Vituo vya afya Vinne na zahanati kumi.
Vifaa tiba vilivyotolewa na Serikali katika hospitali ya Wilaya Nkasi Mkoa wa Rukwa |
Wilaya ya Nkasi imepokea vifaa tiba na dawa vyenye thamani ya shilingi Bilioni 1.8, kwa ajili ya Hospitalii ya Wilaya, Vituo vya afya Vinne na zahanati kumi.
Mkuu
wa wilaya ya Nkasi Peter Lijualikali amesema wamepokea mashine za kisasa za
Mionzi, CT SCAN mashine pamoja na vifaa vya vipimo mbalimba vya magonjwa
amesema
kuwa baada ya serikali kukamilisha ujenzi wa hospitali ya wilaya na vituo vya
afya sambamba na zahanati serikali sasa imetimiza ahadi yake ya ununuzi wa
vifaa tiba na dawa katika wilaya Nkasi
Mkuu
huyo wa wilaya alisisitiza kuwa serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais
Dkt,Samia Suluhu Hassan iliahidi kuboresha huduma za afya na sasa hayo ndiyo
matokeo yake na kubwa ni hjili la kupatikana kwa vifaa tiba vya kisasa.
Mkurugenzi
mtendaji wa wilaya Nkasi Williamu Mwakalambile kwa upande wake alidai kuwa ujio
wa vifaa tiba hivyo vya kisasa unamfanya yeye kuwapeleka wataalamu kwenye
mafunzo zaidi juu ya matumizi ya vifaa hivyo na kwa kuanzia ataanza na
wataalamu wawili.
Alisema
kuwa lengo lake ni kuwa na wataalamu 8 waliopata mafunzo kwa kipindi cha miaka
3 na kuwa ana uhakika kuwa kama kama wataalamu wa vifaa hivyo watakuwepo kuna
uwezekano mkubwa wa jamii kupata huduma bora ukilinganisha na siku za nyuma.
"vifaa
hivi vya kisasa vinaendana na utaalamu wa kutosha hivyo halmashauri
itahakikisha inawapeleka wataalamu wetu kwenye mafunzo na ndani ya miaka mitatu
tutahakikisha wataalamu wanapatikana na kubwa ni tija katika huduma za afya kwa
jamii" alisema
Awali
mganga mkuu wa wilaya Nkasi Benjamini Chota alianisha vifaa vilivyopokelewa
kuwa ni vifaa vya mionzi,CT Scan,Ex-Ray,kifaa cha tiba ya meno,kifaa cha kupima
damu (Blood test machine) vifaa vya tiba ya macho na vipimo vingine vya kisasa
vya magonjwa mbalimbali.
Alisema
kuwa hospita ya wilaya pekee ilipokea Mil.900 na baadae serikali ilipeleka
milioni 900 kwa ajili ya kununua vifaa vingine na katika mgawanyo wa hiyo
fedha vituo 4 vya afya navyo vimenunuliwa vifaa vya afya pamoja na zahanati 10.
katibu
wa CCM wilaya Nkasi Robert Mwega alidai kuwa ujio wa vifaa tiba hivyo vya
kisasa ni sehemu ya ilani ya CCM ya kuhakikisha huduma bora za afya
zinapatikana na jamii inakuwa salama.
Hospitali ya wilaya Nkasi imekamilika kwa gharama ya ujenzi wa zaidi ya shilingi Bil.1.8 na kuifanya jamii kuwa na uhakika wa huduma za kiafya.